KAYA 5'876 ZA NUFAIKA NA MFUKO WA TASAFU AWAMU YA TATU.



KAYA 5'876 ZA NUFAIKA NA MFUKO WA TASAFU AWAMU YA TATU.

Wilayani Tarime mkoania Mara ni Miongoni mwa wilaya 161 Tanzania Bara na Visiwani zinazotekeleza mpango wa kunusuru kaya Maakini kupitia mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF ambapo wilayani Tarime Mkoani Mara kaya 5876 zimeweza kunufaika na mfuko huo kwa asilimia kubwa.


Wakiongea na Mkuu wa Mkoa wa Mara Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Gwitiryo ambao wamenufaika na mradi huo walisema kuwa kwa kiasi kikubwa mradi huo umeweza kuwasaidia kubadili maisha huku baadhi yao wakianzisha miradi mbalimbali ya "Ujasiliamali na kuweza kununua mahitaji ya wanafunzi wa shule.
Baadhi ya familia tulikuwa hatuwezi kula milo ya siku mbili lakini baada ya kupata hizi fedha zimeweza kusaidia familia zetu na fedha hizi zimeweza kuwafikia walengwa hivyo tunatoa shukrani zetu kwa Serikali kwani imeweza kutambua uwepo wetu sisi watu wanaotokana na kaya maskini" walisema.


Akiongea na Wananchi ambao wananuifaika na Mradi huo kwa Nyakati tofauti katika kijiji cha Gwitiryo na Magabari Mkuu wa Mkoa Kapten Mstaafu Asser Msangi alisema kuwa hizo fedha  zinazotolewa wananchi hao wazitumie vizuri kwa kuazisha miradi mabalimbali ikiwemo ufugaji wa kuku na ujasiliamali mdogo mdogo kwa lengo la kujipatia kipato na siyo kutumia katioka matumizi tofauti na makubaliano ya mradi huo.
"Ukifuga kuku kuanzia  kumi na kufuata kanuni bora kutoka kwa wataalamu mbalimbali baada ya mwaka mmoja utakuwa na kuku wengi ambao ukija kuisha mradi huu kwa miaka mitatu utakuwa na kuku wengi na umaskini utaondokana nao"  alisema Msangi.


Hata hivyo Mkuu wa mkoa huyo aliwataka viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime kuweka mpango wa kuanzisha VICOBA vinavyotokana na wananchi walioingizwa katika mradi wa watu kutoka kaya Maskini ili waweze kudunduliza fedha zao kutokana na bihashara yao ndogo wanayoifanya kwa lengo la kujikomboa huku Halmashauri ikianzisha vitaru vya miche yenye kuzaa kwa Muda mfupi na kuwagawia wananchi ikiwemo Parachichi, Papai na Matunda Mengine na kutoa Elimu juu ya upandajina kuwashauri wananchi hao kujiunga na mifuko ya Bimaya ya Afya.


Kwa Upande wake Mratibu wa kuratibu mpango wa kunusuru kaya Maskini Wilayani Tarime Antony Magoti alisema kuwa Halmashauri ya Mji wa Tarime Mradi huo unatekelezwa katika mitaa22 huku Halmashauri ya Tarime Vijijini ukitekelezwa katika vijiji44.


Magoti alisema kuwa Tarime Jumla ya shilingi 259,573,500.00 huku kiasi cha shilingi 234 664,931.82 kwa ajili ya malipo ya walengwa Tsh 2,621 ,954,.55 kwa ajili ya usimamaizi ngazi ya kijiji  na kiasi cha shilingi 24,908,568.18 kwa ajili ya nusimamizi ngazi ya wilaya.


Aidha Mratibu wa mradi huo ngazi ya Wilaya Bw Magot alizitaja changamoto zinazowakabili kuwa ni baadhi ya walengwa kushindwa kijitokeza wakati wa malipo, uhaba wa magari kwa ajili ya malipo vijijini, na kuchelewa kukamilika kwa malipo  kutokana na kukatika mara kwa mara mtandao  wa mfumo wa malipo Epicor.

Hata hivyo ametaja mikakati waliyonayokuwa ni  kuanza kwa maandalizi mapema huku wakiepusha ucheleweshaji wa uchukuaji fedha banki na kuwasisitiza watendaji wa vijiji kutoa taarifa mapema ili ziwafikie walengwa wote kufika siku ya malipo.
                                                                  .........Mwisho......
Powered by Blogger.