WAZIRI KABAKA,NYAMBARI NYANGWINE OUT KURA ZA MAONI ,DC KANGOYE, KEMBAKI WAPETA.
Picha ya Mshindi wa kwanza jimbo la Tarime Mjini Michael Kembaki akisalimiana na wananchi baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo jioni hii |
WAZIRI wa ajira na Kazi Gaudensia Kabaka aliyekuwa anawania Ubunge Jimbo la Tarime Mjini na Mbunge Nyambari Nyangwine aliyekuwa anawania Jimbo la Tarime wamepigwa chini ambapo jimbo la vijijini aliyeongoza ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha Christoper Kangoye na Jimbo la Tarime Mjini Michael Kembaki.
Akitangaza matokeo Mkurugenzi msaidizi wa Uchaguzi Wilaya ya Tarime amabye pia ni Katibu wazazi Wilayani Humo Matius Lugora alisema kuwa kwa Jimbo la Tarime jumla ya kura zilizopigwa ni 35,254, kura halali zilizopigwa ni kura elfu 34,612 na zilizoharibika 642.
Lugora amesema jimbo la Tarime waliotangazania ni 8 ambapo Christoper Kangoye aliibuka mshindi kwa kura 15,928,akifatiwa na John Gimunta 12,205,Nyambari Nyangwine 2,714,Lucus Maricha 1,653, Charles Machage 998,Pius Marwa 590,Maseke Muhono 401, na Paulo Matongo 119.
Lugora ameongeza kuwa Jimbo la Tarime Mjini jumla ya kura zilizopigwa ni kura 74,68,halali zilizopigwa ni 7,339 zilizoharibika 129,wagombea walikuwa sita ambapo Michael Kembaki aliibuka na ushindi kwa kura 3,908,akifatiwa na Gaudensia Kabaka kura 2,411,Philipo Nyirabu 517,Ditu Manco 316, Brito Burure 98 na Jonathan Machango 95.
Akitoa shukrani Christoper Kangoye aliwashukuru wananchama kwa kumpa kura za ushindi nakwamba wamwombee ili jina lake lirudi kwakuwa lengo lake ni kuwasaidia wananchi wa Jimbo la Tarime huku Michael Gimunta akisema yuko tayali kushirikiana na yeyote atakayeletwa kama mgombea Ubunge.
Aidha wakati wagombea wakitoa shukrani zao Nyambari Nyangwine hakuonekana ndani ya ukumbi wa ccm,pia katika uchaguzi ziliibuka changamoto katika kura za maoni kwa nafasi ya Udiwani ambapo Kata ya Bumera Katibu Mwenezi wa Kata Deus Alois alisema kuna kuna wafuasi wa baadhi ya wagombea walikuwa wanapiga kampeni kwenye vituo kushawishi wapiga kura.
John Gimunta ambaye awali jina lake lilikatwa na kisha kurejeshwa alisema kuwa licha ya wenzake kuanza kuzungushwa mapema kabla yake lakini ameshika nafasi ya pili nakwamba amegundua anakubalika kwa wananchi,ambapo watangazania wengine wote walisema kuwa watamuunga mkono atakayeteuliwa makao makuu.
Naye mshindi wa jimbo la Tarime mjini ambaye amemugalagaza gaudensia kabaka Michael Kembaki ambaye ni Mkurugenzi wa Memolia Foundation iliyopo Arusha alisema kuwa wao waendelee kushirikiana huku wakiwa wamoja kwa lengo la kukivusha chma cha mapinduzi huku akisema kuwa tazoidi kushirikiana na viongozi wote kwa lengo la kuletea wananchi maendeleo
Aidha Kembaki amesema kuwa atazidi kuboresha suala zima la michezo kwani hapo awali amekuwa akianzisha ligi kwa lengo la kuwainua vijana na kuwaendeleza endapo atateuliwa na mchakato wa vyama vyote ataweza kushirikiana na wananchi wote ipasavyo.