Gaudensia kabaka, Nyambari Nyangwine wakanusha tuhuma dhidi yao.

Picha ya Mbunge wa jimbo la Tarime Nyambari Nyangwine akikanusha tuhuma ya jana dhidi yake na Mama Kabaka kuhusu kugushi Kura Maoni ambazo zilitarajiwa kufanyika jana .
                            Gaudensia kabaka, Nyambari Nyangwine wakanusha tuhuma dhidi yao.

Waziri wa ajira na kazi Mama Gaudensia kabaka na Mbunge wa jimbo la Tarime Nyambari Nyangwine wakanusha tuhuma dhidi yao zilizokuwa zinawakabili kuwa wao wameusika katika kutengeneza kura feki ambazo zilikamatwa jana zikiwatayari zimeisha wekewa alama ya vema kati ya wagombea hao wanaowania jimbo la Tarime Vijijini na Mjini  saualaambalo wamekanusha  lilipelekea kuharishwa kwa uchaguzi huo hivyo basi  wagombea hao wawili kati ya Nyambari Nyangwine Gaudensia Kabaka wamekanusha suala hilo huku wakidai kuwa hizo ni njama ambazo zimeandaliwa na baadhi ya wagombea wenzao ambao wanataka kuwachafua kisiasa.

Wakiongea na waandishi wa habari Waziri wa ajira na kazi  Mama Gauendensi kabaka amedai kuwa tuhuma hizo hazina ukweli wowote ndani yake na zimemusikitisha sana kama mama anayewania kiti cha ubunge jimbo la Tarime Mjini suala ambalo linazidi kuonesha mfumo dume

Aidha mama kabaka amesema kuwa yeye ni kiongozi mkubwa ambaye hawezi kujiusisha na kugushi nyaraka zozote kwani maamuzi ya kuchagua kiongozi yako kwa wanachama pamoja na wananchi
"Mimi ni kiongoizi mkubwa wa kitaifa siwezi kufanya kitendo hicho cha aibu jakuwa nimesikitika sana na tayari wamevumisha kuwa mimi nimekimbilia kenya kwani nimeuya mtu"alisdema Mama kabaka.

Mama kabaka amezidi kulaani kitendo hicho huku akitupia lawama ofisi ya Chama wilaya kupitia Mwenyekiti wake Rashidi Bugomba huku akidai kuwa yeye ni waziri hawezi kujiusisha na suala la kugushi bali maamuzi yako kwa wapiga kura wataweza kuchagua kiongozi wanayemtaka

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Tarime Nyambari Nyangwine ambaye pia ameusishwa kwenye tuhuma hiyo amesema kuwa siasa za Tarime zimejaa chuki na Uraghai na suala hilo limetokea baada ya kuona wagombea hao wawili wanakubalika katika jamii.

"Tarime kuna siasa za chuki zenye uraghai ndani yake nadhani wameamua kufanya hivyo baada ya kuona sisi tunakubalika kwa jamii na pia walitaka kutuchafulia lakini taratibu zitafuatwa kwa lengo la kuleta maelewano ndani ya chama" alisema Nyambari.

Hivyo Nyangwine alitumia nafasi hiyo kuwataka wananchi waendelee kuwa na mshikamano huku wakiangalia ni kiongozi yupi ambaye anawafaa na waweze kufanya maamuzi yaliyosahii kwa lengo la kuleta maendeleo kupitia majimbo yote mawili.

Aidha Nyangwine aliongeza  kuwa Kuna nguvu Nyingi ndani ya chama hicho kuwa jimbo wanataka lilweze kurudi katika upinzani kwa lengo la kuendelea kutenda maovu yao waliyoyazoea akidai kuwa kwani jimbo hilo alilitoa mikononi mwa wapinzani hivyo hana budi

Kipindi naingia madarakani jimbo la Tarime lilikuwa upinzani nikaweza kulikomboa sasa kwa sasa hata ndani ya Chama kuna baadhi ya viongozi wanatushika mikono pia kuna nguvu kubwa ya kutaka jimbo liweze kurudi tena kambi ya upinzani alisema Nyambari.

Powered by Blogger.