145,288 WATARAJIA KUPATA HUDUMA YA MAJI.


145,288 WATARAJIA KUPATA HUDUMA YA MAJI.
Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya  mwaka 201 2 wakazi wa manispaa ya Musoma wapatao 145,288 ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 4 wanatarajia kupata huduma ya maji ifikapo Feburuari mwaka kesho kutoka katika chanzo kikubwa cha maji yanayorokana na ziwa mvictoria kupitia vituo vya Mwisenge, Bweri  na Mutex.
Akisoma taarifa ya mradi wa ujenzi wa  Miundombinu ya maji safi na usafi wa mzingira (MUWASA) Manispaa ya Musoma Mkurugenzi mtendaji Gantala Said kwa Naibu wa waziri wa maji  amesema kuwa Kituo kikubwa cha Mwisenge kinazalisha majiasilimia98 ya maji yote nayanyotumika katika manispaa ya Musoma.
Aidha Gantala  aliongeza kuwa Miundombinu ya sasa inahudumia asilimia76ya wakazi wa  manispaa ya Musoma.
Amesema kuwa mradi huo unaojengwa  unagharamiwa na szerikali ya Tanzania  na serikli ya Ufaransa kupitia shirika la (Afd) kwa gjhalama za fedha za kitanzania shilingi Billioni 44 pale uatakapookuwa umekamilika.
Hata hivyo Mradi huo umelenga kufanya kazi zifuatazo, Ujenzi wa chanzo kipiya cha maji,  ujenzi wa chujio na mtambo wa kisasa wa kutibu maji, ujenzi wa matanki mapya mawili yenye jumla ya ukubwa wa mita za ujazo 5,500, ujenzi wa mfumo mpya wa  mabomba ya usambazaji wa maji  na kuunganisha mfumo uliopo .
Sambamba na hayo Said ameataja mafanikio yatakayotokana na mradi huo kuwa ni kuongezeka kwa uzalishaji wa maji kutoka mita za ujazo12,000 ambazo ni za sasa kwa siku hadi 36,000 kwa siku, ubora wa maji kwa wananchi na kupunguza milipuko ya magonjwa, huku huduma ya utoaji maji  safi itaongezeka kutoka wastani wa saa20 nakufikia saa24.
Pia alizitaja chanagamoto zinazowakabili kuwa ni pamoja na kubadilika kewa ghalama za umem,e kila mara, madeni ya taasisi za serikali likiwemo jeshi la polisi Magereza Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Hospitali ya Mkoa na Manispaa ya Musoma  ambapo kwa sasa deni limefikia shilingi Millioni 400,ikiwemo na uharibifu na uchafuzi wa vyanzao vya majina miundombinu ya maji na kucheleweshwa kwa hati miliki za maeneo ambayo wanawekeza kwa sasa.
Kwa upande wake Naibu waziri wa maji Amos Makall
amesema kuwa nia ta serikali ni kuhakikisha inatatua chanagamoto ya ukosefu wa maji hapa Nchini na kuboresha Miundo mbinu ya maji kikamilifu.
  Hata hivyo makala amewataka wananchi kulinda vyanzo vya maji pamoja na miundo mbinu ambayo itakuwa imewekwa hukua akitoa shukrani kwa niaba ya serikali kwa Nchi za waisani ambazo zinendeleza juhudi ya kusaidia Tanzani.
........MWISHO.......
 


 

 
Powered by Blogger.