Picha ya mwenyekiti wa chadema wilaya ya Tarime Lukas Ngoto akirudisha fomu jana ya kuwania jimbo la Tarime Mjini ni katika ofisi ya chadema Wilaya.
Wanao wania ubunge Tarime mjini na
vijijini wafika 11 chadema.
Katika
mchakakato uliopo wa kuwania uongozi kupitia ngazi mbalimbali ukiwemo
Ubunge Udiwani na Urais Wilayani Tarime
Mkoani Mara mpaka sasa walijitokeza kuwania ubunge baada ya jimbo kugawanya
wamefikia 11.
Aidha watia
nia hao kwa upande wa Ubunge Jimbo la Tarime Mjini waliotanagaza nia ni Watano
ambao ni Lukas Ngoto Mwenyekiti wa chama
Wilaya Esther Matiko Mbunge wa Viti
maalumu Mkoa wa Mara Chadema , Charles
Werema , Maritinus Joseph na Christopher Chomete. Huku jimbo la Tarime Vijijini
akiwa ni Jonh Heche aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Taifa , Piter Bhusene, Moses Yomami Mwenyekiti wa
Baraza la Vija Wilaya ambaye pia ni Mwanasheria kaanda ya Serengeti , Joanes
Manko, Fabian Mwita na Prosper Nyamuhanga huku jumla wakiwa kumi namoja,
Akirudisha
fomu ya kuwania ubunge jimbo la Tarime Mjini Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo CHADEMA Lukas Ngoto amesema kuwa ameamua kuwania kiti hicho kwa
lego la kuwawakilisha wananchi wote.
Kupitia
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Wilayani Tarime Mkoani Mara Thobias Elias Ghati chama hicho kimesema kuwa kikotayari
kushirikiana na wagombea wote waliotangaza kuwania jimbo la Tarime Mjini na
Vijiji kwa lengo la kupata kiongzi bora ambao watawatumikia wananchi kwa lengo
la kuleta Maendeleo ndani ya Wilaya ya Tarime Mjini na Tarime Vijijini huku
katibu huyo akitaja mnamo 23 julai mwaka katika ukumbi wa chuo cha ualimu
kutafanyika upigaji wa kura z maoni ili kupata viongzi wawili watakao peperusha
bendera ya chama hicho upande wa jimbo la Tarime Mjini na Vijijini,
Sanjari na
hayo kwa leo Mbunge wa viti maalumu kupitia chadema Mkoa wa Mara Esther Matiko
anategemea kupokelewa na watanzania huku akirejea majimboni kwa lengo la
kuongea na watanzania na badae atakuwa na mkutano wa hadhara katika viwanja vya
soko la rebu wilayani hapa. Kwa lengo la kuongea na wananchi kuhusu msitakabari
wake na vipaumbele kwani naye ni mmoja
kati ya wanaowania jimbo la Tarime Mjini na ni mwanamke pekee aliyedhubutu kati
ya waliojitokeza 11.
|