Masurura FC bingwa kombe la Sabega cup
Kulia ni mdhamini wa ligi hiyo Sabega Cup 2015 Fredy Sabega akikabidhi kapten wa Timu ya Masurura Fc baada ya kuilaza Kemange Fc kichapo cha bao1-0 kupitia mkwaju wa penaliti na kuibuka washindi na kujinyakulia kitita cha shilingi laki Nne.
Masurura
FC bingwa kombe la Sabega cup
Tarime
LIGI ya iliyopewa jina la Sabega imemalizika huku timu
ya Masurura ikiibuka bingwa msimu wa 2015 kwa usindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi
ya Kemange FC kwenye mchezo wa fainali uliyochezewa kwenye uwanja wa Kemange
shule ya msingi, halmashauri ya mji wa Tarime mkoani Mara.
Bao pekee la timu ya Masurura lilifungwa na
Jaliwa Alkard dakika ya 72 kwa mkwaju wa penaliti baada ya mchezaji huyo
kutendewa madhambi eneo la hatari la lango la timu ya Kemange ambapo
mwamuzi mwenye beji ya FIFA Sophia Mtongori aliamua kutengwa kwa penaliti hiyo.
Mshindi huyo wa kwanza (Masurura)
waliibuka na kitita cha sh, 400,000 na kikombe cha thamani y ash,
300,000, mshindi wa pili (Kemange) aliibuka na sh, 300,000 na kikombe cha
thamani ya sh, 200,000huku mshindi wa tatu Nyamonkanga aliibuka na sh, 150,000
na kikombe chenye thamani y ash, 100,000.
Nahodha wa timu ya Masurura Ignas Ponsiano alisema
kuwa ilikuwa ni halali yao kuibuka mabingwa wa ligi hiyo kwa kuwa tangu
michuano hiyo inanze juni 23 na kumalizika julai 12 hawakuwahi kupoteza hata
mchezo mmoja kutokana na hali hiyo ushindi huo ulikuwa ni wao.
Kwa upande wake kocha wa Kemange FC Samwel Mwita
ambao walikuwa wenyeji wa uwanja huo ameiambia blog hii kuwa amepokea ushindi wa namba mbili kama
changamoto kwake kama kocha na kuwa waonyeshwa kuwa bado wanahitajika kufanya
juhudi kwa ili kuwa mabingwa msimu ujao.
Naye mdhamini wa ligi hiyo Fredy Sabega alisema
mwaka wa nne ameona wachezaji wazuri tofauti na miaka mingine ambayo ilimfanya
akataka kukata tamaa hivyo viwango vyao vya kisoka kufikia katika
kiwango ambacho wanaweza kuuzika katika timu kubwa za kitaifa.
“Lengo langu ni kuona vijana wanaibua vipaji vya soka
katika kata ya Nyandoto nimeona ndoto nyangu inaenda kutimia kwani huu ni
mwaka wangu wa nne tangu nilipopata wazo la kuwakusanya vijana ili kuleta umoja
na kuwafanya wasiingie kwenye masuala ya uhalifu viwango vyao vya soka
vimepanda… wanaohitaji vijana kwa ajili ya timu zao nawaomba wafike katika kata
ya Nyandoto” alisema Sabega.
Sebaga aliongeza kuwa ratiba rasimi tayari ipo katika
chama cha mpira wilaya hivyo kila mwaka kutakuwepo na mashindano kwa lengo la
kukusanya vijana kwa pamoja kwa lengo la kuepukana na vishawishi kama vile
Ngono zembe madawa ya kulevya hivyo muda mwingi watautumia katika michezo.
Mwisho.