MAKADA 109 WARUDISHA FOMU YA KUGOMBEA NAFASI YA UDIWANI TARIME/RORYA.
Tarime.
MAKADA 109 wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo CHADEMA wiki hii wamerudisha Fomu ya kugombea nafasi ya Udiwani
Wilayani Tarime na Rorya mkoani Mara.
Akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake katibu baraza la Wazee Chadema wilaya Tarime Samsoni Sanda amesema
kuwa kati ya 105 waliorudisha fomu kwa jimbo la Tarime 46 ni viti maalumu.
Aidha Sanda ameongeza kuwa
mchakato huo ulianza Juni 19 hadi kukamilika Julai 10 mwaka huu ambao
siku hiyo ndiyo ilikuwa mwisho wa kurudisha fomu za kuwania kuomba nafasi
ya Udiwani.
Kwa upande wa jimbo la Rorya makada
4 akiwamo Diwani Thomasi Partrick Lisa na wenzake
wawili wamerudisha fomu ya kugombea nafasi ya udiwani kukamilisha idadi ya
watia nia Tarime na nRorya kufikia 109.
Thomasi Patrick amesema kuwa
akifanikiwa kuteuliwa na kupitishwa na chama chake atahakikisha barabara ambazo
zinaleta kero ndani ya kata yake ya Kitembe pamoja na Wilayanzima ya Rorya
barabara zinapitika kwani katika awamu nyingine diwani huyo amechukua fomu ya
kuwania ubunge wa jimbo la Rorya sanjari na kuongeza ufanisi wa ufaulu kwa
wanafunzi.
Wengine waliorudisha fomu ya
kugombea nafasi ya udiwani kata ya Kitembe kupitia CHADEMA ni pamoja na Kerina
Oyuma na Mery Thomasi Makodede Makodede wakata ya Bukwe Wiliamu Otuki kata ya
Roche alisema Gradus Festo Ndira mwenyekiti CHADEMA Kata ya kitembe.
Mmoja wa watia nia Mtoto wa marehemu
Chacha Wangwe ambaye aliwahiu kuwa mbunge wa jimbo la Tarime kupitia CHADEMA,Zakayo
Chacha Wangwe aliwambia waandishi wa habari kuwa kama chama chake kama
kitamteuwa na kuwa mgombea udiwa ani kata ya Turwa Wilayani Tarime atahakikisha
anashirikiana na wananchi wake kuwaletea maendeleo.
Aidha Zakayo ameongeza kuwa endapo
atafanikiwa kuingia halmashauri atatumia nafasi yake kushawishi madiwani
wenzake kubuni vyanzo vipya vya mapato ili kuingizia halmashauri
fedha ya kuendeshea miradi ya maendeleo kwa wananchi wa Tarime na Tanzania kwa
ujumla.