Picha ya viongozi wa Balaza la wanawake chadema Bawacha wakiwa katika kaburila Baba wa Taifa Hayati Julius Kambalage Nyerere


Serikali imetakiwa kutunza makumbusho ya Baba wa Taifa Hayati Julius Kambalage Nyerere ili yaendelee kuwepo kwa lengo la kizazi kijapo.
Kauli hiyo imetolewa jana na Naibu katibu mkuu Balaza la wanawake Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kunti Yusuph kwenye ziara ya kutembelea makumbusho uya Baba wa Taifa katika kijiji cha Mwitongo wilayani Butiama.

Naibu hiyo alisema kuwa serikali nimekuwa ikitumia fedha nyingi lakini imesahau kutuna makumbusho ya baba wa taifa katika hadhi ya kimataifa
“Tumetembelea makumbusho ya Baba wetu wa taifa lakini huwezi kuyathaminisha na  yale alikuwa akiyafanya hayati Julius Kambalage” aalisema Naibu.
Naye mbunge wa viti maalumu jimbo la Tarime Mkoania Mara Ester Matiko amezidi kulaani vitendo vya vifo kwa akina mama nakuwataka kuungana pamoja ili kutokomeza vifo hivyo.
“Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ni Mwanamke lakini tunaendelea  kufaliki tunaomba jeshi la polisi kujipanga sawa na si kuja kurekodi mikutano ya Chadema na kushindwa kusaka waoua” alisema Matiko.
Kwa upande wake mbunge wa viti maalumu Grace kiwelu aliwataka wananchi kuondokana na ukabira,pamoja na  udini ili kudumisha Amani, Upendo na Mshikamano.
Katika uhai wa hayati Nyerere alipinga sana ukabira iweje kwa sasa chama cha CCM kishindwe kutetea yale aliyoyaacha Baba wa Taifa.
Hata Mmoja wa kutunza makumbusho hayoBaraka Bwire katika kutoa historia ya Hayati lasema kuwa wanakabiliwa na ukosefu wa fedha ili kuendeleza makumbusho hayo.

“Ruzuku zinatengwa kutoka serikalini lakini zinafika zikiwa zimechelewa na wakati mwingine ufika kidogo na kusababisha ukosefu wa fedha zaq kuendeshea na kuboresha  makumbusho haya” alisema Bwire.
                      ……MWISHO…
Powered by Blogger.