WWF WATOA MAFUNZO KWA VIJANA.
WWF WATOA MAFUNZO KWA VIJANA.
Vijana 25
kutoka wilaya za Mkoa wa maraukiwemo mkoa
wa Mwanza wamepata mafunzo juu ya Utunzaji wa mazingira pamoja na vyanzo vya maji ikiwa ni moja ya kuwapa fursa za kujiajili
wenyewe kupitia vikundi mbalimbali waliyonayo katika wilaya huskaVijaha hao
ambao wamepata mafunzo hayo wametoka wilaya ya Rorya, Musoma Bunda Serengeti na
Mkoa wa Mwanza lengo kubwa ikiwa utunzaji kuwajengea uwezo juu ya utunzaji wa mazingira ususani kupitia mto
Mara.
Shirika hilo
la WWF linalojiusisha na utunzaji wa mazingira
pamoja na uifadhi wa Vyanzo vya maji, Mwakilishi wa Mratibu wa Mradi
Mwasiti Rashid kupitia mwakilishi wa Adah Waigoma alisema kuwa mafunzo hayo
yamekuwa yakitolewa mara kwa mara kwa lengo la kuwajengea vija uwezo wa kuhunda
vikundi na kuviendeleza wenyewe.
“Sisi
tumekuwa tukitoa mafunzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwezesha vikundi vya
ujasiliamali ili viweze kusonga mbelena kujikwamua kiuchumi” alisema waigoma.
Mmoja wa
washiriki katika Mafunzo hayo Usina Dotto kutoka katika Mkoa wa Mwanza kwenye
kikundicha Nyegezi Youth ambapo kikundi hicho
ujiusisha na suala la ufugaji wa kuku na utunzaji wa mazingira elimu
aliyoipata ataenda kuisambaza kwa vijana wenzake ili kuweza kuondokana na
utegemezi.
“Kupitia
mafunzo haya nimejifunza mengi nitazidi kutoa kile nilichokipata kwa vijana
wenzangu ili kuweza kupanua wigo na kushauri vijana wajiunge katika vikundi
mbalimbali ili kuweza kupata msaada wa haraka” alisema Usina.
Naye issa
Juma kutoka Bunda aliongeza kuwa kupitia mafunzo hayo yanayotolewa kwa vijana
kwa lengo la kvijana kutunza mazingira vijana wengi wilayani Bunda Mkoani Mara
wameanza kujishughulisha kwa wingi.,
“Tunahamasisha
vijana wenzetu waendelee kujishughulisha na siyo kusubira ajira kutoka Serikalini”
alisema Issa.
……Mwisho…