Migogoro ya kifamilia chanzo kikubwa kwa mabinti mkufanya bihashara ya kingono
Elieth Samsoni kutoka dawati la jinsia manispaa ya Musoma Mkoani Mara akiwasilisha mada juu ya watoto ambao wamejiingiza katika bihashara ya ngono ni katika kikao cha wadau kilchofanyika leo kwenye ukumbi wa shirika la Center
For Widows and Children Assistance lililopo Mjini Musom
Imebanishwa
kuwa migogoro ni chanzo kikubwa cha usababishi wa watoto wadogo ususani mabinti
kujiingiza katika suala zima la bihashara ya kingono katika wilaya ya Butiama,
Musoma Mjini na Musomavijijini Mkoani Mara, suala ambalo upelekea mabinti hao
kupata mimba za utotoni pamoja na maambukizi ya virusi vya ukimwa na Magonjwa
ya zinaa.
Hayo
yamebainishwa katika kikao cha wadau kwenye ukumbi wa Ofisi za Shirika la
Center For Widows and Children Assistance zilizopo Manispaa ya Musoma
Mkoani Mara kwa kuusisha wadau kutoka
taasisi mbalimbali kama vile, Maofisa ustawi wa jamii, Wasaidizi wa kisheria,
watendaji wa kati , Weneviti wa vijijina Vitongoji, Mashirika ya utetezi wa
haki zabinadamu,Wandishi wa habri na Maofisa kazi kutoka katika wilaya za
Butihama, Musoma mjini na Musoma Vijijini.
Katika
kuchangia mada zilizowekwa mezani wadau hao walisema kuwa Migogoro inapoingila
katika family wazazi upelekea kutelekeza familia na kufanya watoto kujitunza wenyewe
na kupelekea kkujiingiza katika vishawishi vya kingono.
“Baba au
Mama wanapokimbia familia upelekea watoto kujitunza wenyewe suala ambalo
upelekea kuijiingiza katika masuala ya kingono kwa ajili ya kupata kipato cha
kuendesha familia hizo” walisema wadau hao.
Ofisa
Mwandamizi wa shirika la Center For Widows and Childres assistance Ostack Mligo
ambao pia ni wawezeshaji wa mdharo huo alisema kuwa lengo kubwa la kukutanisha
wadau hao ni kuangali namna ya kunusuru watoto ambao tayari wamejiingiza katika
bihashara za kingono Mkoani Mara ili kuweza kuwasaidia
“Lengo kubwa
ni kuona kipi kifanyike, chanzo kikubwa ni nini kwani watoto wetu wanazidi
kuangamia kutokana na bihashara hizi za kingono” alisema Mligo.
Elieth Samsoni
kutoka katika dawati la jinsia katika manispaa ya Musoma alizitaja changamoto zinazowakabili katika
utendaji kazi ili kutokomeza vitendo vya ukatili vinavyozidi kutendeka hapa
nchini alisema kuwa baadhi nya Watendaji wa kata, wenyeviti wa Vijiji, na
Vitongoji wamekuwa wakihamua kesi na kupelekea kupotea kwa ushaidi.
“Sisi dawati
la jinsia na wtoto tukifuatilia kesi za watuhumiwa vijijini wakatimwa kufika
eneo la tukio tunakuta tayari watendaji wa kata vijijina vitongoji wamekaa mezani
na kumaliza kazi” alisema Elieth.
Kwa upande
wake diwani wa kata ya Buhare Lukas
Masige alilahani kitendo cha wenyeviti wa vijiji na watendaji wa kata ambao
wamekuwa mihungu watu na kuzidi
kuwanyanyaja wananchi wao pale wanapoitaji huduma.
Licha ya hayo
wadau walisema kuna aja kubwa ya kuhusisha walimu, Wazazi wote wawili Baba na
Mama katika washa zinazoandaliwa kwani uka na watoto kwa mda mwingi ili kuweza
kutokomeza vitendo vya ukatili vinavyotendeka.
“Mashuleni
walimu ndio walezi wakubwa haebu jaribu kuwashirikisha katika mijadala kama hii
ili kuweza kutimiza ndoto zenu nyie kama asasizisizokuwa za kiserikali ambazo
zimeamua kumkomboa mtoto wa Tanzania” walisema.
……MWISHO…