Wazee wa mila wahapa mbele ya Dc Tarime
Tarime
Wazee wa
mila kutoka koo zote za kabila la Wakurya Wilayani
Tarime Mkoani Mara wamekubaliana kuacha
kukeketa watoto wa kike mbele ya Mkuu wa Wilya
Tarime(DC) John Henjewele nakusema kuwa Wasichana sasa
kupakwa unga ili kuendelea kudhumisha mila zao
Wazee
hao walisema kuwa kuanzia sasa watoto wa kike ambao
wamefikisha umri wa miaka 17 watakuwa wakipakwa unga usoni
kama ishara ya kudumisha mila hiyo kila
inapofika wakati wake
“
Kuanzia sasa mheshimiwa DC hili jambo la ukeketaji
tumelimaliza. Ila sherehe zote zitakuwa zikifanyika
lakini kukeketa hapana”, wazee hao walisema
katika kikao kilichofanyika katika ofisi ya DC Henjewele hivi
karibuni.
Kikao
hicho kilikuwa chini ya uenyekiti wa DC Henjewele na
kiliwezeshwa na Shirika la Jukwa la Utu wa
Mtoto(CDF) kwa ufadhili wa Shirika la Umoja wa
Mataifa la Idadi ya Watu(UNFPA) na Tasisi ya Graca Machel Trust.
Kikao
hicho kilihudhuliwa pia na Mkurungenzi Mtendaji wa Halmashuri
ya Wilaya ya Tarime Athuman Akalama na
maafisa wa polisi kutoka ofisi ya kamanda
wa mkoa wa kipolisi wa Tarime Rorya.
Hata
hivyoWazee hao walisema kila mwaka wamekuwa wakipiga
hatua katika kuitikia wito wa serikali na kuacha kukeketa
watoto wa kike.
“ Miaka ya
hivi karibuni tulikuwa tunaketeka ki-CCM bila kuwaumiza watoto
lakini tumeanza kuwapaka unga ili tu kudumisha mila na sasa
itakuwa ni kupaka unga tu na hakuna kukeketa”, walisema.
“
Leo tumetamka kuwa ukeketaji Tarime hakuna
na hata aliyepanga kutukamata hatatupata tena”, alisema
mmoja wa wazee hao.
Wazee
hao walikubaliana kuanza kusadia kutoa elimu
dhidi ya ukeketaji katika maeneo yao ili kuweza kuwashawishi baadhu
ya wazee ambao wanaendekeza masua;la haya ya kimila.
DC
Henjewele aliwashukuru wazee hao kwa kukubali
kuachana na ukeketaji lakini akaonya kuwa zoezi hilo la
kupaka unga lisije likatumiwa vibaya .
“
Tuiialike na sisi hata kwenye hizo za sherehe za
kupaka unga , zoezi hilo lisiitwe ukeketaji, litafutiwe jina
lingine na kuruhusu watu wapige hata picha ili kuonesha
hakuna ukeketaji tena Tarime na tusije kupata ushadi wa mtoto
kukeketwa”, alisema DC Henjewele.
“
Serikali bado inahitaji msaada wenu wazee wangu ili
tuondakane na aibu hii. Leo mmeifurahisha serikali”, Mkuu huyo wa
wilaya aliawambia wazee hao .
DC
henjewele aliunda kamati maalumu ambayo
itasimamia na kufutilia utekelezaji wa makubaliano katika kikao
hicho ikiwa ni pamja na kuangalia shughuli mbadala zitakazokuwa
zinafanywa na wazee hao baada ya kukubali kuachana na
ukeketaji. Kamati hiyo tayari imeeanza kazi yake.
Mwisho