Isticama walzawa kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Mafundi fc:

picha ya kapten wa Timu ya mafundi fc akikabidhiwa kikombe na OCD wa Tarime Issa Bukuku kwa niaba ya kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi Tarime Rorya Lazaro Mambosasa



Isticama walzawa kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Mafundi fc:

Timu ya Isticama Fc imelazwa kichapo cha bao bao 1-0 katika fainali za michuano ya kembaki Cup zilizokuwa zikiendelea walayani hapa katika uwanja wa shamba la Bibi Serengeti.
Katika mashindano hayo zilizweza mushiriki timu kumi na mbili kwa njia ya mutoano ndipo zilibakia timu sita na kuwa na makundi ya A na B ambapo zilitoka timu mbili Mafundi Fc na Isticama nakuingia fainali.
Katika michuano hiyo timu zote mbili ziliweza kuoneshana ubabe na ndipo dk ya 80 kipindi cha pili mafundi Fc walichungulia nyavu za Isticama kupitia kwa Ibraim sabiro bao ambalo li;lidumu mpaka  dk 90 za mchezo huo zinaisha.
Katika michuano hiyo ya Kembaki Cup2013-2014 mshindi wa kwanza ambaye ni Mafundi Fc walijinyakulia kombe na shilingi laki Tano, Mshindi wa pili laki Tatu ambaye ni Isticama Fc huku mshindi wa pili Kenyamanyori Fc laki mbili.
Michael Kembaki ambaye ni  mdhamini wa michezo alisema kuwa lengo la michezo hiyo ni kuwezesha vijana kujituma katika utendaji wa kazi kupitia michezo.
“Michezo ni burudani kupitia michezo hii vijana watajituma hivyo tutazidi kuboresha michezo kwani hii ni awamu ya pili nikidhamini michezo na mwakani nitaongeza zawadi” alisema Kembaki.
 Kwa upande wake katibu wa chama cha mpira wilayani Tarime(TAFA)  Brandani Mtatiro aliwataka viongozi wa virabu kutumia kanuni 17 za michezo ili kuboresha michezo.
“Viongozi wa virabu wasipotumia kanuni zote za mpira bado changamoto zitzidi kujitokeza” alisema katibu wa chama cha mpira.
Naye  OCD Wa wilaya Issa Bukuku kwa niaba ya kamanda wa polisi Mkoa wa kipolisi Tarime Rorya aliwataka vijana kupenda michezo huku wakizidi kudumisha Amani
“Michezo bila amani haiwezekani hivyo tuendelee kudumishsha Amani ili kuboresha Michezo” alisema.
                                …..Mwisho…
Powered by Blogger.