Ondoeni ukabira, ubinafsi ili kupata Viongozi bora.



Ondoeni ukabira, ubinafsi ili kupata Viongozi bora.

Jamii wilayani Rorya mkoani Mara imetakiwa kuondokana na ukabira ili kuweza kuwapatia fursa viongozi wapya kwa lengo la kuleta Maendeleo ndani ya  vitongoji, Vijiji  na Kata hadi Wilaya.

Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Rorya Samwe Keboye (Maarufu kama namba tatu) kipindi akiongea na wajumbe pamoja na viongozi wa CCM katika ukumbi wa Owan Hotel iloyopo Mji mdogo wa Shirati.

Mwenyekiti huyo alisema kuwa baadhi ya maeneo likiwemo eneo la Ryagati wananchi wamekuwa wakichaguo viongozi kwa sababu ya makabira jambo ambalo linazidi kurudisha maendeleo ya wananchi Nyuma
“Ryagati kuna viongozi wameongoza zaidi ya miaka kumi katika vitongoji na vijiji kwa sababu ya kabira Fulani acheni tabia hizo badirisha viongozi watakaowaletea maendeleo” alisema Mwenyeki.

 Kwa upande wake katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Rorya Fikirini Salimu Masokola alisema kuwa  chama kimewapigania wananchi wamepata mamlaka ya mji mdogo wa Shirati hivyo hawana budi kuchagua viongozi wazuri watakaoongoza mamlaka hiyo na kuleta maendeo.

“Mamlaka hii haikuletwa na Chadema,wala Cuf ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais Jakaya Kikwete chagueni viongozi wazuri watakao endesha mamlaka hiyo” alisema katibu huyo.

Ongujo Wakibara ni mmoja wa wafanybihashara wakubwa na mmilikiwa Owan Hotel katika mji mdogo wa Shirati aliwataka wafanyabihashara kuondokana na utofauti kwa ajili ya kuletea mji huo maendeleo ya haraka.
Aaidha Wakibara alisema kuwa endapo watashindwa kuendesha Mamlaka hiyo watanyanganywa hivyo aliwataka wananchi wote kuunganisha nguvu ya pamoja ili kufanya mapinduzi 

Hata hivyo Zabroni  john na Martha Julius wamezidi kuipongeza serikali ya Tanzania kupitisha Mji mdogo wa Shirati kuwa Mamlaka ya Mji mdogo suala ambalo litasaidia kuongeza kuongeza Mapato ya ndani kupitia mamlakahivyo.
“Sisi kama wananchi na wakazi wa Shirati tumekuwa na kilio cha muda mrefu wa kutafuta mamlaka hii sasa kikubwa ni kuchagua viongozi waliobora ili kuleta maendeleo ya haraka” walisema.

                                         ……MWISHO….
Powered by Blogger.