Ondoeni ukabira, ubinafsi ili kupata Viongozi bora.
"Ondoeni ukabira, ubinafsi ili kupata
Viongoz"
Jamii
wilayani Rorya mkoani Mara imetakiwa kuondokana na ukabira ili kuweza kuwapatia
fursa viongozi wapya kwa lengo la kuleta Maendeleo ndani ya vitongoji, Vijiji na Kata hadi Wilaya.
Kauli hiyo
ilitolewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Rorya Samwe
Keboye (Maarufu kama namba tatu) kipindi akiongea na wajumbe pamoja na viongozi
wa CCM katika ukumbi wa Owan Hotel iloyopo Mji mdogo wa Shirati.
Mwenyekiti huyo
alisema kuwa baadhi ya maeneo likiwemo eneo la Ryagati wananchi wamekuwa
wakichaguo viongozi kwa sababu ya makabira jambo ambalo linazidi kurudisha
maendeleo ya wananchi Nyuma
“Ryagati
kuna viongozi wameongoza zaidi ya miaka kumi katika vitongoji na vijiji kwa
sababu ya kabira Fulani acheni tabia hizo badirisha viongozi watakaowaletea
maendeleo” alisema Mwenyeki.
Kwa upande wake katibu wa chama cha mapinduzi
wilaya ya Rorya Fikirini Salimu Masokola alisema kuwa chama kimewapigania wananchi wamepata mamlaka
ya mji mdogo wa Shirati hivyo hawana budi kuchagua viongozi wazuri
watakaoongoza mamlaka hiyo na kuleta maendeo
“Mamlaka hii
haikuletwa na Chadema,wala Cuf ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais
Jakaya Kikwete chagueni viongozi wazuri watakao endesha mamlaka hiyo” alisema
katibu huyo.
Ongujo
Wakibara ni mmoja wa wafanybihashara wakubwa na mmilikiwa Owan Hotel katika mji
mdogo wa Shirati aliwataka wafanyabihashara kuondokana na utofauti kwa ajili ya
kuletea mji huo maendeleo ya haraka.
Aaidha Wakibara
alisema kuwa endapo watashindwa kuendesha Mamlaka hiyo watanyanganywa hivyo
aliwataka wananchi wote kuunganisha nguvu ya pamoja ili kufanya mapinduzi
Hata hivyo Zabroni john na Martha Julius wamezidi kuipongeza
serikali ya Tanzania kupitisha Mji mdogo wa Shirati kuwa Mamlaka ya Mji mdogo
suala ambalo litasaidia kuongeza kuongeza Mapato ya ndani kupitia mamlakahivyo.
“Sisi kama
wananchi na wakazi wa Shirati tumekuwa na kilio cha muda mrefu wa kutafuta
mamlaka hii sasa kikubwa ni kuchagua viongozi waliobora ili kuleta maendeleo ya
haraka” walisema.
……MWISHO….