ASISITIZA SUALA LA AMANI WILAYANI TARIME:
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Bw: Benedict Olekuyan amesisitiza suala zima la Amani wilayani Tarime Mkoani Mara ili kuweza kujiletea Maendeleo .
Ametoa kauli
hiyo jana katika Ufunguzi wa wa Kongamano la Siku Maalumu ya Polisi lililofanyika katika
Ukumbi wa CMG Motel Wilayani Tarime Mkoani Mara uku zikiwasilishwa Mada
mbalimbali ili kuweza kuleta Mahusiano Mazuri baina ya Jeshi la Polisi na
Wananchi.
Mgeni rasmi
ambaye ni katibu Tawala wa Mkoa Wa Mara aliongeza kuwa Maendeleo ya Mkoa,
Nchi,Wilaya,Tarafa,Kata,na Kijiji hayawezi kuwa Endelevu kama suala zima la
Amani halitakuwepo pamoja na Ushirikiano Mzuri baina ya Wananchi na Jeshi la
Polisi.
“Uwekezaji
Mkubwa na Mdogo,Bihashara,Kilimo,huduma za jamii, Miundombinu hayangewezekana
kama kusingekuwepo kwa Amani” alisema
Katibu Tawala.
Aidha Katibu
tawala huyo alitumia fursa hiyo kutoa rai kwa Waandishi wa habari kutumiaFursa
zao vizuri kwa lengo la kuandika Mazuri ya Tarime ili na simkuandika habari za
Uchchezi tu kuleta “Waandishi wa habari Musiandike Mabaya ya Tarime tu jaribu
kuandika hata mazuri yanayofanyika ndani ya Wilaya” alisema.
Kwa
upande wake kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi Tarime/Rorya Justus Kamugisha
aliongeza kuwa jamii iondokane na suala zima la kujijengea dhana kuwa jeshi la
polisi ni adui bali wazidi kushililkiana
vyema ili kuweza kuleta Mahusiano Mazuri.
“Sisi
tumezaliwa na Nyinyi lakini tunafanya kazi za Serikali acheni kututenga
ushilikiano kwanza ilituweze kusukuma gurudumu la Maendeleo changamoto
zinazoikumba jeshi la Polisi tutazidi kutatua” alisema Kamanda wa Polisi.
Aliongeza kuwa
jeshi la polisi linakumbwa na Changamoto mbalimbali hivyo kwa kushilikiana na
Wadau mbalimbali kama Vile NG’OS,CBO,
Taasisi za dini zitumike vizuri kushauri jeshi la polisi kwa leng la kubresha na kudumisha Amani .
Hata hvyo
katika kuwasilisha Mada yalitajwa Mapendekezo kuwa wafanyabihashara Wakubwa
wajaribu kununua CCTV Camera na kufunga Maeneo husikia kwa lengo la kuzidi
kudumisha Suala la ulinziwa Mali zao kwani Jeshi la Polisi haliwezi
kutimiza yote kwa wakati Mmoja ikiwa ni
pamoja na kuandaliwa kwa daftari la kudumu kwa Wakazi kwa lengo la kuwa na
kumbukumbu.
Sanjari na
hayo jeshi la polisi limetaja Changamoto zinazowakumba kama vile,Upungufu wa
vitendea kazi kama vile Magari,Pikipiki,kilinganisha na Ukubwa wa Maeneo ya
Utendaji kazi, Ukosefu wa ajila kwa vijana unapelekea vIjana kujiingiza katika Vitendo
Viovu,Jeshi la polisi kuhudumia watu wengi mfano askali mmoja kuhudumia
Wananchi Mianne hadi Miatano.
Mwisho kikao
hicho kwa kushilikisha Taasisi mbalimbali, Wanasiasa, Viongozi wa dinina Wananchi
wa kawaida kwa kushilikiana na Jeshi la Polisi wameazimia mambo yafuatayo na
kuhaidi kuyafanyia kazi,Serikali iongeze bajeti kwa jeshila polisi ili kuweza
kupata Vitendea kazi,Kuanzishwa mfuko wa pamoja wa ulinzi Shirikishi,kudhibiti
ajali za barabarani ikiwa ni pamoja na kuta Mafunzo ya Usalama barabarani kwa
waendesha Pikipiki (Boda bada) na Wananchi kutii Sheria bila Shuruti.
……MWISHO….