Baada ya kukaa naye na kumtathimini kwa takribani wiki mbili, hatimaye
klabu ya Yanga imefikia makubaliano ya imemsainisha mkataba kocha wake
mpya Mwinyi Zaheri ambaye ni raia wa DR Congo.
Yanga ambayo imepokonywa ubingwa wa ligi kuu na Simba SC, imekubaliana
na mtaalam huy o wa ufundi kwa mkataba wa miaka miwili ya kuifundisha
Yanga ambayo inacheza makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Zahera amechukua rasmi mikoba ya Mzambia George Lwandamina aliyekuwa
kocha mkuu wa kikosi cha Yanga baada ya kuondoka kimyakimya kurejea kwao
Zambia katika klabu yake ya zamani, Zesco United.
Zahera ni kocha msaidizi wa timu ya taifa ya DRC, The Leopard na mwenye
uzoefu wa kufundisha soka katika bara la Ulaya pamoja na Afrika.
Licha ya kusaini mkataba huo, Zahera ameondoka nchini kwenda kwao Congo
kwa majukumu ya kukitumikia kikosi cha timu ya Taifa ya Congo na baadae
atarejea nchini kuendelea na Yanga.