“Wazee wa Mila Tarime sasa tunaona Ukeketaji ni Kero”
Mzee
wa Mila kutoka Koo ya Butobori akieleza jinsi wazee hao walivyoungana
kwa lengo la kupiga Vita Suala la Ukeketaji kwa Mtoto wa Kike wilayani
Tarime Mkoani Mara ambapo amesema kuwa sasa ifike Mwisho suala la
ukeketaji limalizike kwani limekuwa Kero huku akiomba Sister Stella
Mgaya ambaye ni mkurugenzi wa shirika la ATFGM Masanga Tarime kuweka
Mikakati ya ujenzi wa Kanisa katika kata ya Nyandoto ili Wananchi
wabadilike baada ya kutambua Mwenyezi Mungu.
'Kwa Sababu Mtu
ambaye anajua suala la Dini huwezi kumwambia aende kwenye Mizimu kwa
sababu anatumikia Mwenyezi Mungu Makanisa hapa kwetu ni Muhimu sana"
alisema Mzee huyo.
Wananchi wa Kijiji cha Masurula Kata ya Nyandoto koo ya Butobori Wakipatiwa Elimu na Madhara ya Ukeketaji kwa Mtoto wa Kike.
Wazee wa Mila kutoka Koo ya Butobori wakiwa katika Kikao hicho
Abel
Gechaine ambaye ni Mratibu wa Huduma ya Afya na Ustawi wa Jamii Wilaya
ya Tarime akitoa Elimu ya Madhara anayoyapata Wakati wa Kijingua
Mwanamke aliyekeketwa.
Sister
Stella Mgaya kutoka shirikal la ATFGM Masanga ambao wameungana na Wazee
hao kwa lengo la kuzunguka Koo12 na kutoa Elimu juu ya Madhara ya
Ukeketaji kwa Mtoto wa kike.
Mwita
Nyasibora kutoka Koo ya Butimbaru akitoa Elimu na kutaja Miiko ambayo
wameondoa Wao kama Wazee wa Mila ili Msichana ambaye hajakeketwa
aonekana anathamani kama aliyekeketwa katika jamii inayomzunguka.
Baadhi
ya wananchi wakichangia hoja akatika Mkutano huo wa hadhara huku
wakiomba Wazee hao kusimamia Msingi na siyo kutoa Matamko na Kisha
kukeketa Watoto wa kike.
Nchagwa
Mtongori ambaye ni Mwenyekiti wa Wazee wa Mila Muungano wa Koo12 Kabila
la Wakurya Wilayani Tarime Mkoani Mara akitoa Elimukwa Wananachi hao
.....Tazama video hapa Chini walichikisema Wazee.......