Wananchi Tarime walia na Mipaka ya hifadhi ya Serengeti ,Viongozi wa CCM...


Wananchi
Kutoka Vijiji Vinavyopakana na Hifadhi ya serengeti katika Kata ya
Nyanungu Wilayani Tarime Mkoani Mara wakitoka Maeneo ambayo yamewekewa
alama za kutenganisha Mipaka ya hifadhi  hiyo na Wanaanchi yaani Beffer.

Wananchi
hao wamedai kuwa kitendo cha Serikali kwa kushirikiana na Watu wa
TANAPA Kwenda kuweka mipaka hiyo bila ya kuwashirikisha hawajapendezwa
nacho huku wakiomba Serikali kuu kuingilia kati juu ya Mgogoro huo ili
kubaini Ukweli.



"Sasa
maeneo haya kuna wazee wamekaa zaidi ya Miaka 50 kwa sasa unasema
wahame wataenda wapi kijiji kizima kitaenda wapi kata ya Nyanungu,
Goronga na Gibaso serikali itatupeleka Wapi Walisema" Wanaanchi hao.


Kamati
ya Siasa CCM Wilaya ya Tarime wameweza kufika eneo la mipaka hiyo na
kujionea hali halisi huku wakiomba Wanaanchi hao kuwa watulivu ili suala
hilo liweze kupatiwa ufumbuzi.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya
Tarime Daud Marwa Ngicho amesema kuwa tayari ameishaongea na waziri
Mwenye dhamana na atafika eneo huska kwa lengo la kutoa tamko la
Serikali.

,,,,,,,,,,Tazama Picha za Matukio Tofauti,,,,,,,,,,,

Wananchi wakisiliza Viongozi wa CCM Wilaya ya Tarime Mkoani Mara .



Viongozi wa kamati ya Siasa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Tarime wakisilikia Kilio cha Wananchi wa kata ya Nyanungu.


Mwenyekiti
wa CCM Wilaya ya Tarime Daud Marwa Ngicho akiongea na Wakazi wa
Nyanungu ambapo amesema tayari suaala hilo wameishalifikisha ngazi ya
Juu na litafanyiwa kazi.

Katibu
wa CCM Tarime Khamis Mkaruka Kura akiongea na Wananchi ambapo amesema
kuwa suala la kuweka Mipaka ni sahihi lakini jambo la kushirikisha
wananchi kupitia Mkutano wa hadhara ni la Msingi sana.

Mwenyekiti
wa UVCCM Wilaya ya Tarime Godfrey Franacis akiongea na wananchi ambapo
amesema kuwa wao kama Chama kupitia kamati ya Siasa wameamua kuingilia
kati ili kubaini Ukweli na kusaidia wanaanchi hao.

Baadhi ya Alama ambazo zimewekwa na Serikali ya Wilaya ya Tarime kwa kushirikiana na TANAPA Katika Maeneo ya Nyanungu.

Baadhi ya Wananchi wakitoa Kilio chao kwa Viongzo wa CCM kupitia Kamati ya Siasa Wilaya ya Tarime.





Peter
Busene Mkazi wa Nyamwaga akiongea na Wananchi hao jinsi alivyosaidia
baadhi ya  wananchi amabo walikamatwa kuhusiana na Mgogoro huo.


Wananchi wakielekea Maeneo ya mipaka na Viongozi wa CCM


Wakipima Mita kutoka Maeneo yanye Alama Beffer kuelekea Bikoni za zamani zilizowekwa na Mkoloni.




Wanaanchi wakianagali baadhi ya alama ziliazowekwa.






,,,Tazama Video Wananchi walichokisema pamoja na Majibu ya Viongozi wa CCM Kamati ya Siasa Wilaya ya Tarime,,,
Powered by Blogger.