Polisi Wanne Watiwa Mbaroni kwa Kumjrehi Mke Wa Mwenyekiti Jijini Mwanza Wakati wakiwa Wamelewa
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Ahmed
Msangi ametoa amri kukamatwa kwa askari polisi wanne wa Kituo Kikuu cha
Polisi Nyamagana kutokana na asakri hao kumjeruhi kwa risasi mke wa
Mwenyekiti mtaa.
Kamanda Msangi amesema polisi hao tayari
wametiwa mbaroni kwa kumjeruhi kwa risasi mguuni Bi. Editha Ntobi ambaye
ni mke wa Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Majengo Mapya uliopo katika
Kata ya Mabatini jijini Mwanza.
Msangi amesema polisi hao
wanatuhumiwa kufyatua hovyo risasi zaidi ya 10, kuharibu mali za raia
lakini pia wanadaiwa kufanya matukio hayo kutokana na kulewa wakati
wakiwa kwenye doria kinyume na utaratibu wa kazi yao.
Bi Editha
Ntobi ambaye ni majeruhi wa kupigwa risasi amelazwa katika hospitali ya
Rufaa Bugando iliyopo jijini Mwanza kutokana na kuvuja kwa damu nyingi
kufutia tukio hilo.