REAL MADRID, BARCELONA WANAVYOANZA KUTENGENEZA MAMILIONI KUPITIA JEZI MPYA
Tayari
vigogo wa soka la Hispania na duniani kote, Real Madrid na Barcelona
wameishatoa jezi zao mpya kwa ajili ya msimu wa 2017-18.
Suala
sasa ni bei au mauzo ya jezi hizo yatakuwaje. Jezi za Real Madrid
kupitia kampuni ya Adidas na Barcelona kupitia Nike, tayari zimepangiwa
bei.
Zile za Madrid hazijaanza kuuzwa lakini bei yake itakuwa kati ya euro 99.95 ambayo ni uero 100 hadi 129.5 ambayo ni euro 130.
Barcelona wao wameingiza mzigo sokoni, bei inaanzia euro 100 hadi 150 na tayari wameanza kuuza.
Hata hivyo kutokana na mafanikio makubwa ya Madrid hasa kwa kubeba ubingwa wa Ulaya, jezi zao zinaweza kupanda bei.
Pia wameweka utaratibu kuwa kama unataka jezi, bukta na soksi zake, unalipa euro 208.
Madrid na Barcelona ni kati ya timu zinazoingiza kiasi kikubwa cha fedha kutokana na mauzo ya jezi.
