EXCLUSIVE: SPORTPESA NA SINGIDA UNITED MAMBO SAFI, "NDOA" RASMI LEO




Kampuni ya michezo ya kubahatisha ya SportPesa, imeendelea kuonyesha imepania kusaidia michezo kwa upande wa soka baada ya kukubaliana na Singida United.


Sportpesa imefikia makubaliano ya kuidhamini Singida United na leo inatarajiwa kuingia mkataba wa kuidhamini klabu hiyo.

Habari za uhakika kutoka ndani ya Singida United ambayo imepanda Ligi Kuu Bara msimu huu, zimeeleza makubaliano hayo yatasainiwa leo mbele ya waandishi wa habari.

“Sasa ni uhakika kuwa mkataba unasainiwa na kila kitu kipo vizuri,” kilieleza chanzo.

Uamuzi wa SportPesa kuidhamini Singida United unaonyesha kiasi gani imepania kusaidia michezo na si Simba na Yanga pekee kama wengi ambavyo walifikiri awali.



Tayari SportPesa imeingia mkataba wa miaka mitano kuzidhamini timu kongwe nchini za Yanga na Simba ambazo kila moja kwa muda huo itaondoka na Sh bilioni 5.
Powered by Blogger.