BANDA ASISITIZA ANAONDOKA KWENDA SAUZ, LAKINI....
Beki kiraka wa Simba, Abdi Banda amesema anakwenda nchini Afrika Kusini kucheza soka la kulipwa.
Hata hivyo, Banda hajasema anakwenda timu gani na yeye amesisitiza anayejua ni meneja wake.
Maneno
hayo ya Banda, yanafuatia yale aliyoandika mtandaoni akiwaaga mashabiki
wa Simba baada ya mechi ya fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Mbao
FC na Simba kushinda kwa mabao 2-1.
Hata hivyo, mashabiki wengi wamekuwa wakieleza kuwa Banda anataka kuwapa presha viongozi wa Simba ili kuharakisha usajili wake.
Lakini Banda amesema: “Ni kweli naondoka, nakwenda Afrika Kusini kujaribu bahati yangu. Maana sina mkataba.
“Kama
viongozi wataniita nitasikiliza, na mimi nitawaeleza mahitaji yangu
halafu tutaona. Kama sivyo, basi nitaangalia nini kitaendelea huko
mbele.’”