|
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt.
Harrison Mwakyembe (kushoto) akipokelewa na Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA), Dkt. Herbet wakati alipowasili katika taasisi
hiyo kuzindua vitendea kazi 4 Aprili, 2017 Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.
|
|
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt.
Harrison Mwakyembe (mwenye tai nyekundu) akiwa ameongozana na Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) Dkt. Herbet Makoye pamoja
na viongozi wengine na watendaji wa TaSUBA wakati alipowasili katika taasisi
hiyo kuzindua vitendea kazi 4 Aprili, 2017 Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.
|
|
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt.
Harrison Mwakyembe akiwa ameongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sanaa
na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA), Dkt. Herbet Makoye pamoja na watendaji
mbalimbali wa Wizara na wa taasisi hiyo kuelekea kuangalia maeneo mbalimbali ya
taasisi 4 Aprili, 2017 Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.
|
|
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo
(TaSUBA), Dkt. Herbet Makoye akimuonyesha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe jinsi maji ya bahari yalivyoharibu kingo
za taasisi hiyo wakati alipowasili katika taasisi hiyo kuzindua vitendea kazi 4
Aprili, 2017 Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt.
Harrison Mwakyembe akionyeshwa baadhi ya vifaa vilivyomo ndani ya Studio za
Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) wakati alipowasili katika
taasisi hiyo kuzindua vitendea kazi 4 Aprili, 2017 Wilayani Bagamoyo Mkoani
Pwani.
|
|
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt.
Harrison Mwakyembe akipiga nyimbo kwa kutumia kinanda ndani ya moja ya Studio
za Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) wakati alipowasili katika
taasisi hiyo kuzindua vitendea kazi 4 Aprili, 2017 Wilayani Bagamoyo Mkoani
Pwani.
|
|
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt.
Harrison Mwakyembe akiongea na
wafanyakazi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA), wageni waalikwa
pamoja na wanafunzi wa taasisi hiyo kabla ya uzinduzi wa vitendea kazi vya
taasisi hiyo 4 Aprili, 2017 Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani. |
|
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt.
Harrison Mwakyembe akizindua rasmi vifaa vya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni
Bagamoyo (TaSUBA), 4 Aprili, 2017 Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.
|
|
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt.
Harrison Mwakyembe akipokea zawadi za picha za kuchora toka kwa Mkurugenzi wa
Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA), Dkt. Herbet Makoye wakati
alipowasili katika taasisi hiyo kuzindua vitendea kazi vya taasisi hiyo 4
Aprili, 2017 Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt.
Harrison Mwakyembe (mwenye tai nyekundu) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi
wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSUBA) pamoja na watendaji wengine wa Wizara
mara baada ya kuzindua vitendea kazi vya taasisi hiyo 4 Aprili, 2017 Wilayani
Bagamoyo Mkoani Pwani.
|
|
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt.
Harrison Mwakyembe (mwenye tai nyekundu) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi
wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSUBA), Watendaji waWizara pamoja na wageni toka nje ya nchi
mara baada ya kuzindua vitendea kazi vya taasisi hiyo 4 Aprili, 2017 Wilayani
Bagamoyo Mkoani Pwani.
|
(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM)
Na Lorietha Laurence.
Waziri wa Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amezindua Vifaa vya kufundishia vyenye thamani ya shilling
100 kwa ajili ya Taasisi ya Sanaa na
Utamaduni Bagamoyo(TaSUBa) vitavyowawezesha wanafunzi kujifunza kwa vitendo namna ya kutengeneza
picha jongefu.
Akizungumza wakati wa
uzinduzi huo leo Wilayani Bagamoyo, Dkt.Mwakyembe amesema kuwa vifaa hivyo ni
muhimu katika maendeleo ya kitaaluma ya wanafunzi wa Taasisi hiyo katika
kuwaongezea ujuzi katika vitendo na baadaye kuwa watendaji bora na makini.
“Vifaa hivi ni tija
katika kuhakikisha kuwa wanafunzi wanajifunza kwa vitendo na hivyo kuzalisha
watu wenye taaluma zenye tija na zenya kuleta matokeo chanya kwa ajili ya maendeleo nchi”alisema
Mhe.Dkt.Mwakyembe.
Aliongeza kwa kuhaidi
kuwa atahakikisha viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri na Mabalozi wanapata
fursa ya kuitembelea TaSUBa ili wajionee
kwa macho hazina kubwa waliyonayo katika
kukuza na kuendeleza sanaa na utamaduni.
Aidha aliupongeza viongozi
na walimu wa TaSUBa kwa jitihada wanazozifanya za kutoa elimu kwa vijana jambo ambalo linawajengea
uwezo wa kujiajiri kupitia taaluma ya sanaa
hivyo kuondoa utegemezi na kukuza uchumi
wa nchi.
Naye Katibu Tawala wa
Wilaya ya Bagamoyo Bibi Erica Yegela kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo alisema
Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo(TaSUBa) ipo kwa ajili ya maslahi ya
Watanzania wote na hivyo wanakaribishwa kujiunga na kujifunza sanaa,utamaduni
na uandaaji wa vipindi.
Kwa Upande wake
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Dkt. Herbert
Makoye ameishukuru Serikali kwa kutoa fedha za maendeleo kiasi cha shilling
millioni 100 amabazo zimefanikisha kununua vifaa vya kufundishia kwa vitendo.
“Tunaishukuru Serikali kwa kutupatia kiasi
hiki cha fedha ambapo kwa kiasi kikubwa kimefanikisha manunuzi ya vifaa hivi vya kufundishia na huu ni mwanzo mzuri nasi
tunaahidi kutumia ipasavyo katika kuzalisha wanataaluma hodari” alisema Dkt.
Makoye.
Aliongeza kwa kusema kuwa licha ya kufanikiwa katika
kununua vifaa kumekuwapo na changamoto mbalimbali zinazoikabili- Taasisi hiyo
ikiwemo upungufu wa wafanyakazi huku wengi wao wakiwa wamestaafu,uhaba wa ofisi
za waalimu na wafanyakazi pamoja na
miundo mbinu chakavu.