Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya MUUNGANO WA Tanzania Kassim Majaliwa akimpongeza Makamu wa
Rais wa Simba SC Geofrey Nyange Kaburu mara baada ya kununua picha ya Timu ya
Serengeti Boys, wakati wa hafla ya kuchangia timu ya hiyo jana Jijini Dar es
Salaam. Hafla hiyo iliandaliwa na TFF kupitia Kamati ya Hamasa ya Serengeti
Boys kwa lengo la kuchangia fedha za kugharamia mahitaji ya timu hiyo
inayoshiriki Kombe la AFCON U17 nchini Gabon. Kutoka kushoto ni Rais wa TFF
Jamal Malinzi, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison
Mwakyembe, Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa ya Serengeti Boys Charles Hillary na
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Omary Singo.
|