UWANJA UKICHELEWA, SINGIDA HAWATAIONA SINGIDA UNITED LIGI KUU MWANZONI
Inaonekana
kama zoezi la ukarabati wa uwanja wa Namfua mjini Singida umekuwa
ukienda kwa mwendo wa kobe jambo ambalo linaweza kuwakosesha uhondo
mashabiki wa mkoa huo.
Mashabiki
wa soka mkoani Singida wanaweza kukosa raha ya kushuhudia mechi za Ligi
Kuu Bara wakati Singida United ikiwa imereja katika ligi hiyo.
Kocha
Hans van der Pluijm, lazima atataka maandalizi ya uhakika na pia mechi
kuchezwa katika eneo ambalo lina uhakika jambo ambalo linaweza
kusababisha Singida united kuhama mkoani hapo.
Taarifa za ndani zimeeleza kwamba, Singida United wanaweza kuhamia katika mkoa mwingine wa Dodoma ambao upo kanda ya kati.
"Kocha anataka uwanja ambao timu inaweza kucheza soka safi, huenda
mwanzo timu ikahamia Dodoma halafu baada ya ukarabati itarejea Singida,"
kilieleza chanzo.
Lakini taarifa zinaeleza juhudi za makusudi zimekuwa zikifanyika
kuhakikisha Singida United inaanza mechi zake za Ligi Kuu Bara kwenye
Uwanja wa Namfua.