TRL YAANZISHA SAFARI ZA TREN YA MIZINGO DAR - DODOMA.
Na James Salvatory
Shirika la reli
Tanzania (TRL) jana limeanzisha safari za treni ya mizingo (FLAG OFF)
ya shirika la mpango wa chakula duniani (WFP) lenye lengo la
kuhudumia wateja kwa kiasi na muda unaoridhisha na kufikisha bidhaa
kwa walaji wake.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi huo Jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa TRA,
Masanja Kadogos,a alisema kihistoria huduma hiyo ilikuwepo tangu enzi
za shirika la reli Tanzania TRC na katika mwaka 2004 ilikuwa
imeshasafirisha jumla ya tani 400,723 za WFP na kuanzia mwaka 2006
ukashuka kutoka tani 66,994 hadi tani 846 kwa mwaka 2015.
Aidha alisema
kuwa moja kati ya changamoto iliyopo ni ukosefu wa vichwa vya Tren vya
kutosha na mabehewa Hata hivyo baada ya kujipanga na kuihakikishia
huduma zinakamirika kusafirishia tani 7000 za mahindi kupeleka katika
ghala kuu la WFP iliyoko Kiota Dodoma .
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa bodi ya TRL, John Kondoro, alisema kuwa tangu mwaka 2000
hii ni mara ya pili shirika hilo linasafirisha mizigo na kwa sasa
wamesafirisha mzigo mkubwa na hii ikiwa ni faida maana inaongeza faida
kwa shirika na kwa kufika hatua hiyo imani kubwa inajengeka kwa wadau
kwa kazi hii inayofanyaka.