TANZANIA STARS FOOTBALL CLUB, KLABU MPYA YA SOKA YA WATANZANIA INAYOIBUKA KWA KASI NCHINI CHINA
Na Mwandishi Wetu, China
Kwa
miaka ya hivi karibuni, ulimwengu wa soka umeshuhudia mapinduzi makubwa
yaliyoletwa na uwekezaji wa hali ya juu wa fedha nyingi
kupitiliza;hii imefanya vijana wadogo kununuliwa na kulipwa mishahara
mikubwa kuliko vipaji vyao wenyewe.
Wakati
dunia ikiendelea kushangaa pesa waliyonunuliwa Paul Labile
Pogba,Gonzalo Higuain,Gareth Bale,John Stones,Raheem Sterling na wengine
wengi, wachina wao ndo kwanza kila kukicha wanavunja benki na
kuwatunuku watu hundi kubwa pasi na mifano na ndo sababu kubwa kwa nini
hivi karibuni tumeshuhudia majina makubwa yakitoka klabu kubwa na
ligi bora kokote kule duniani na kwenda China.
Zamani
tuliamini na kuona wachezaji ambao umri umewatupa kama kina
Anelka,Drogba, Xavi n.k ndo wangekata kauli kuja kucheza ASIA KAMA
Dubai,Qatar,Oman ila leo imekuwa tofauti wachezaji wa umri mdogo na tena
ambao walikuwa na nafasi ya kutengeneza historia kubwa kwenye ramani
ya mpira ulaya kama Oscar, Paulinhno, Axel Witsel, Jackson
Martinez,Graziano Pelle, Olunga na wengine wengi wakija CHINA kwa nguvu
ya pesa za usajili na mishahara minono wanayotoa wachina.
Ni
wazi vijana wengi watakimbia ulaya kuja huku,na yote hii wanafanya kwa
agizo la raisi wao mheshimiwa Xi Jinping ambaye duru lake linataka
kufikia 2050, China iwe inaongoza katika viwango vya FIFA katika mpira
wa miguu,japo kwa maono na mtazamo wangu hawauhitaji 2050, bali
watahitaji kuwa na subira hadi 2025 tu, kufikia hapa na imani dunia
itashuhudia mapinduzi makubwa katika ligi ya China.
Si
lazima wawe wanaongoza katika viwango vya Fifa vya dunia bali tu hii
ligi itakuwa imepewa jicho la dunia, itapata wawekezaji wengi na taswira
pana ya kibiashara kama ilivyo ligi ya Uingereza, vijana wengi
watajenga kiu ya kutaka kucheza huku na hadi ikifka 2050, China itakuwa
imepiga hatua kubwa kimpira kama mataifa mengine kama Uingereza,
Hispania, Ufaransa n.k.
Kwa kuyaelewa haya,Watanzania waishiyo China wakaamua kuanzisha timu yao maarufu kama TANZANIA STARS FOOTBALL CLUB(T.S.FC).
TANZANIA STARS FOOTBALL CLUB(T.S.FC):
T.S.FC ni kifupi cha TANZANIA STARS FOOTBALL CLUB
Ni
taasisi ya kukuzia vipaji inayojitegemea iliyoanzishwa na watanzania
wachache wanaosoma Kaskazini mwa China katika jimbo la Liaonning, mji wa
Shenyang; mji mkongwe katika historia ya China. Ni saa tano tu kwa
treni ya umeme (bullet) kutoka mji mkuu wa China, Beijing na pamepakana
na Korea Kaskazini.
HISTORIA FUPI YA T.S.FC
Ni
taasisi inayojihusisha na kukuza vipaji vya mpira wa miguu.Taasisi hii
ilianzishwa tarehe 1/11/2013 katika chuo kikuu maarufu hapa Shenyang,
SHENYANG AEROSPACE UNIVERSITY (S.A.U).Suala la kuanzisha taasisi
lilikuja kama wazo baada vijana watano; ABDULWAHID ISMAIL BITEGEKO,
NASSOR KOMBO, HAGGAI JAMES,YUSUPH ISMAIL BITEGEKO na AGGREY JOSEPH
MWAKASITA kukaa chini na kuona kuna haja ya kuanzisha taasisi hii.
Ilianza
na wachezaji 10 tu na kwa mtiririko huu ndo taasisi imepiga hatua hadi
hapa ilipo hivi sasa. Mpaka kufikia mwaka 2012,hiki chuo SHENYANG
AEROSPACE UNIVERSITY (S.A.U) ambapo ndo kila kitu kilipoanzia Kulikuwa
na watanzania wawili tu ambao wote hawakuwa wakipenda mpira na
ikawalazimu watu wa hapa kusubiri hadi mwaka 2013.
Wakati
watanzania walipoanza kuja huku rasmi hususani Kaskazini mwa China hasa
ukizingatia Watanzania na wageni wengi wanaokuja China hupendelea
kwenda Kusini mwa China kwenye miji kama Guangzhou,Shanghai n.k
Haikuwa
safari rahisi kuisimamisha hii taasisi leo ilipo na hasa ukizingatia
kwa kipindi hicho,mwaka 2013,bado masuala ya mpira kwa watu weusi
hayakuwa yakipewa kipaumbele kuanzia na vyuo hadi na mji huu,bado
wagheni hasa waafrika walikuwa wakiathiriwa na ile dhana ya kuwa mtu
mweusi alikuwa bado binadamu mgeni huku.
Hakukuwa
na mazingira sahihi ya kuanzisha taasisi ya kimpira huku ikabidi kupiga
moyo konde na kwa mapenzi ya mchezo huu pendwa duniani tena wakiwa 10
tu,ikaanzishwa taasisi ya mpira wa miguu ambayo kwa kipindi kile
ilionekana kama kitu kigeni sana hata kwa wanafunzi wenzao wa kigeni
ambao wengi walikuwa wabezaji na wakosoaji tu.
Wengi
watashangaa kivipi na wachezaji 10? Wachezaji 10 na kipa tulikuwa
tunakodisha kutoka kwa nchi zingine na hawa Watanzania 10 hawakuwa wote
wakitokea chuo cha SHENYANG AEROSPACE UNIVERSITY (S.A.U),wengine
walitoka karibu kama SHENYANG MEDICAL COLLEGE na CHINA MEDICAL
UNIVERSITY. Mwanzoni walicheza mechi za kirafiki na timu za vyuo kwa jua
mataifa mengi hayakuwa yamejipanga kwa wakati huo.
Baada
ya kucheza michezo kadhaa ndo mataifa kama Nigeria,Ghana,Zambia,Russia
na wengine walipofuatia baada ya kuona ni kwa kiasi gani tumefanikiwa.
Mwaka wa 2014 ulikuwa wa matunda mengi na ndipo hii timu ndogo ilipozaa
taasisi baada ya kupata vijana wengi ima waliokuja kusoma au hata kuishi
huku, ambapo mpaka sasa taasisi imekuwa na ina wachezaji yapata 60
ikiwa na uongozi wa juu, kocha, benchi zima la ufundi wakiwemo madaktari
na washabiki wengi tu ambao wote wanafanya kazi kwa ajili ya kujitolea
na kwa hisani ya taifa mama la Tanzania.
MAFANIKIO YA TAASISI HII;
- • Imekuwa taasisi ya kwanza ya mpira ya waafrika kuanzishwa na kujisimamia yenyewe.Imeweza kusimamia watanzania yapata 60 na wachezaji takribani 12 kutoka Kenya, Rwanda, Burundi, Uganda, Djibouti, Somalia .
- • Japo si kitega ajira rasmi ila tumeweza kutoa ajira zisimo rasmi kwa wachezaji wetu kwa kupata timu za kuchezea hususani za wachina na nchi zingine ambao wamekuwa wakikodi wachezaji kutoka hapa kwa malipo wanayopewa wachezaji wao wenyewe.
- • Tumeanzisha mashindano ya MATAIFA AFRIKA na KOMBE LA DUNIA ya huku kwa hisani yetu wenyewe ambayo kwa mafanikio kabisa yametimiza miaka miwili Tangu kuanzishwa na mara zote tumekua washindi wa pili.
- • Tumeitunza heshima ya Tanzania na leo kila mmoja anajivunia kile wanachofanya watanzania huku na tumechaguliwa kuwa TAASISI BORA YA MICHEZO mara mbili na jumuiya ya watanzania wanaoishi CHINA chini ya UBALOZI WA TANZANIA NCHINI CHINA.
Moja ya mashindano yaliyoandaliwa na taasisi ya T.S.FC
DIRA YA TAASISI;
Dira
kuu ya taasisi ni kuifanya hii taasisi kuwa moja ya taasisi kubwa siku
za usoni,kuipeleka timu kushiriki LIGI kuanzia madaraja ya chini hadi
ligi kuu na pamoja na kuwa kitovu kikuu cha kuwapa nafasi vijana wa
kitanzania kuonyesha uwezo wao na hata kupata timu za kwenda kufanya
majaribio.
KWA MAWASILIANO
whatsapp +8615566140449
Instagram; tanzaniastars
Email; tanzaniastars@gmail.com