|
Kaimu
Kamishna wa Elimu kutoka Wizara ya
Elimu Sayansi na Teknolojia Bw. Nicolas Bureta akizungumza na wadau wa
Elimu ya Watu Wazima wakati wa warsha iliyolenga kuibua mbinu na
mikakati ya kusaidia kufuta
ujinga wa kutojua kusoma, kuandika na kuhesabu kwa vijana na watoto.
Kulia ni
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Dkt. Fidelice
Mafumiko.
Warsha hiyo ilifanyika hivi karibuni Jijini Dar es Salaam. |
 |
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Dkt. Fidelice
Mafumiko akizungumza na wadau wa sekta ya elimu wakati wa warsha ya utoaji maoni
kuhusu mpango wa utoaji elimu kwa makundi maalum ya vijana na watoto walio
chini ya umri wa miaka 17. Kushoto ni Kaimu Kamishna wa Elimu kutoka Wizara ya Elimu
Sayansi na Teknolojia Bw. Nicolas Buretta. Warsha hiyo ilifanyika hivi karibuni
Jijini Dar es Salaam.
|
 |
Naibu Mkurugenzi wa Taaluma, Utafiti na Ushauri kutoka
Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) Dkt. Kassimu Nihuka akimkaribisha Mkurugenzi
Mkuu wa Taasisi hiyo, Bw. Fidelice Mafumiko (wa pili kulia) kutoa taarifa
kuhusu malengo ya semina kwa wadau wa elimu iliyofanyika hivi karibuni Jijini
Dar es salaam.
|
Kaimu Kamishna wa
Elimu kutoka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Bw. Nicolas Buretta (katikati)
akisisitiza jambo kwa washiriki wa semina hiyo. Warsha hiyo ilifanyika hivi
karibuni Jijini Dar es Salaam.
 |
.Baadhi ya washiriki wa warsha ya wadau wa elimu iliyoratibiwa
na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Tanzania (TEWW) wakifuatilia hotuba ya Kaimu
Kamishna wa Elimu kutoka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Bw. Nicolas Buretta
(hayupo pichani). Warsha hiyo ilifanyika hivi karibuni Jijini Dar es Salaam.
|
 |
Kaimu Kamishna wa
Elimu toka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Bw. Nicolas Buretta (katikati) akiwa
kwenye picha ya pamoja na washiriki wa semina ya wadau wa elimu iliyoratibiwa na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Tanzania iliyofanyika hivi karibuni Jijini Dar es Salaam.
( Picha na Frank Mvungi )
Frank Mvungi
Taasisi ya Elimu ya Watu wazima Tanzania (TEWW)
imedhamiria kuondoa changamoto ya Watanzania wasiojua kusoma na kuandika hapa nchini
hasa vijana walio chini ya umri wa miaka 17.
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Kamishna wa Elimu kutoka
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Bw. Nicolas Buretta wakati akifungua warsha
ya siku moja ya wadau wa Elimu iliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
“Tunalenga kuwafikia watoto ambao hawajapata
kabisa fursa ya kupata elimu kwa sababu ya umaskini au mazingira na pia
tunalenga kuwafikia watoto wote walio na umri chini ya miaka 17” Alisisitiza
Buretta.
Akifafanua Buretta amesema dhamira ya Serikali ni
kuhakikisha kuwa kila mtoto anapata haki ya kupata elimu bora ili kuzalisha
wataalamu wenye ujuzi, uwezo na weledi watakaosaidia kujenga uchumi wa viwanda.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu
Wazima Dkt. Fidelice Mafumiko alisema kuwa mpango huo unatoa kipaumbele kwa
wale waliokosa elimu kupitia mfumo rasmi
ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano kuhakikisha kuwa kila
mtoto anapata elimu.
“Dhamira ya Taasisi ya Elimu ni kuhakikisha kuwa
kunakuwa na mfumo nyumbufu utakaowezesha Watanzania wote wanapata elimu iwe
katika mfumo rasmi au usio rasmi” Alisisitiza Mafumiko.
Kwa upande wake Mtaalamu wa Elimu kutoka UNICEF
Dkt. Ayoub Kafyulilo alisema kuwa maktaba za Kata zitasaidia kuongeza ari ya kujisomea
miongoni mwa vijana na jamii kwa ujumla.
Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) iko chini
ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na ina jukumu la kuendeleza Elimu ya
Watu Wazima (EWW) na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi nchini.A
|