SIMBA YAENDELEA KUJIFUA MORO, YAELEZWA MORALI YA KUICHAKAZA AZAM FC IKO JUU
Kikosi
cha Simba chini ya kocha wake, Joseph Omog kimeendelea na mazoezi mjini
Morogoro kujiandaa na mechi yao ya keshokutwa ya Kombe la Shirikisho
jijini Dar es Salaam.
Simba itakuwa mwenyeji wa Azam FC kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mechi inayotarajiwa kuwa ngumu.
Mratibu
wa Simba, Abbas Ally ‘Gazza’, amesema wanaendelea na maandalizi vizuri
na uongozi unatimiza majukumu yake kuhakikisha vijana wanafanya vizuri.
“Kila
kitu kinakwenda vizuri, kila kitu kipo kamili na hakika vijana
wanajituma kweli. Lengo ni kufanya vizuri katika mechi hiyo,” alisema.
“Kila mmoja wetu anajua ni mechi ngumu na muhimu, hivyo kikubwa ni kuendelea kujituma kwa juhudi zaidi.”