SERIKALI YAWATAKA WAAJIRI KUJISAJILI KWENYE MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI (WCF)
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu Jenista Mhagama amewataka waajiri nchini kujitokeza kwa wingi
kujisajili katika Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (Workers Compesation
Fund – WCF) kwa ajili ya kuwawezesha waajiriwa kupata mafao pindi
wanapoumia,kuugua au kufariki wakiwa kazini.
Akizungumza
wakati wa maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Mahali pa kazi duniani
yaliyofanyika Aprili 28,2017 kitaifa katika viwanja vya Chuo Kikuu cha
Ushirika mkoani Kilimanjaro,alisema bado kuna mwamko mdogo kwa waajiri
kujisajili katika mfuko wa WCF.
“Kama
waajiri hawatajisajili katika mfuko wa fidia kwa wafanyakazi bado
mtaendelea kuwa na shida ya kuwatibu wafanyakazi wao,lakini pamoja na
kujali afya za wafanyakazi pia mjiandae kuwalipa fidia wanapoumia wakiwa
kazini”, alisema Mhagama.
“Serikali
inathamini sana juhudi zenu kama waajiri katika kuajiri
wafanyakazi,niwaombe sana Chama Cha Waajiri nchini tushirikiane katika
kuongeza hamasa ya kujisajili kwenye mfuko wa fidia kwa wafanyakazi”,aliongeza Mhagama.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Matibabu na Tathmini kutoka Mfuko
wa Fidia kwa Wafanyakazi – WCF, Dkt. Abdulssalaam Omary
Alisema
mwitikio mpaka sasa kati ya waajiri 23,000 waliowabaini 700 pekee ndiyo
wamesajiliwa katika mfuko huo hivyo kuiomba serikali isaide kuhamasisha
waajiri wajisajili kwenye mfuko huo.
Katika
hatua nyingine Dkt. Omary alisema katika kipindi cha Mwezi Julai,2016
mpaka Machi 31,2017 wamepokea taarifa ya matukio 478 kutoka kwenye
maeneo ya kazi.
Alisema
kati matukio hayo 478,matukio ya ajali ni 454,magonjwa sita na vifo 18
katika maeneo ya viwandani,migodini na vyombo vya usafiri ambapo
waliopata ajali huduma ya fao la matibabu
Aidha
alisema mfuko huo unatoa mafao 7 ambayo ni mafao ya huduma ya
matibabu,malipo ya ulemavu wa muda,malipo ya ulemavu wa kudumu,malipo ya
anayemhudumia mgonjwa,huduma za ukarabati na ushauri nasaha,huduma za
mazishi na malipo ya wategemezi.
Angalia picha za matukio yaliyojiri katika banda la WCF katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro
Angalia picha za matukio yaliyojiri katika banda la WCF katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu Jenista Mhagama (aliyevaa nguo nyeupe) akisalimiana kwa
kushikana mkono na Afisa Mahusiano wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi -
WCF Zaria Mmanga alipotembelea banda la WCF wakati wa maadhimisho ya
siku ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi mwaka 2017 katika viwanja vya
Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro
Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano WCF, Laura Kunenge akimkaribisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama katika banda
la WCF wakati wa maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi
mwaka 2017 katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi mkoani
Kilimanjaro
Mkurugenzi
wa Huduma za Matibabu na Tathmini kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi
– WCF, Dkt. Abdulssalaam Omary akiwasilisha mada fupi kuhusu Mfuko huo
ambapo alisema walengwa wa mafao yanayotolewa na WCF kuwa ni wafanyakazi
wa sekta ya umma na binafsi ambao wataumia au kuugua kutokana na kazi
walizoajiriwa nazo.
Dkt. Abdulssalaam Omary aliongeza kuwa walengwa wengine wa mfuko huo ni wategemezi wa mfanyakazi atakayefariki kutokana na ajali au ugonjwa uliotokana na kazi.Katikati ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama akisikiliza mada fupi katika banda la WCF.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama akiuliza swali kwa Mkurugenzi wa Huduma za Matibabu na Tathmini kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi – WCF, Dkt. Abdulssalaam Omary kuhusu mwitikio wa waajiri kujisajili katika mfuko huo ambapo Dkt. Omary alisema bado mwikitio hauridhishi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama akiongea na Mkurugenzi
wa Huduma za Matibabu na Tathmini kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi
– WCF, Dkt. Abdulssalaam Omary.Katikati ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA
Hadija Mwenda
Mkurugenzi
wa Huduma za Matibabu na Tathmini kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi
– WCF, Dkt. Abdulssalaam Omary akitoa ufafanuzi kwa wananchi
waliotembelea banda la WCF kuhusu mfuko huo ambao ni taasisi ya hifadhi
ya jamii iliyoundwa kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha sheria ya fidia kwa
wafanyakazi (sura 263 marejeo ya mwaka 2015).
Kulia ni Afisa Rasilimali Watu kutoka
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi – WCF,Lilian Msaki akitoa elimu kuhusu
mfuko huo kwa wananchi waliotembelea banda la WCF.Alisema lengo la
kuanzishwa mfuko huo ni kushughulikia masuala ya fidia kwa wafanyakazi
wanaoumia,kuugua au kufariki kutokana na kazi wanazozifanya kwa mujibu
wa mikataba ya ajira zao.
Afisa
Mahusiano wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi - WCF, Zaria Mmanga
akielezea kuhusu fao la huduma ya matibabu ambapo alisema pale mwajiriwa
anapoumia au kuugua atapatiwa matibabu na huduma mbalimbali ikiwemo
kupatiwa viungo bandia,malipo ya dawa,kumuona daktari,huduma za
upasuaji,uuguzi na kurudia matibabu pale inapobidi.
Kulia
ni Mwananchi akiuliza swali kuhusu Fao la Malipo ya Ulemavu wa muda
mfupi na ulemavu wa kudumu kwa Afisa Mahusiano wa Mfuko wa Fidia Kwa
Wafanyakazi - WCF Zaria Mmanga
Afisa
Mahusiano wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi - WCF Zaria Mmanga
akielezea kuhusu msaada wa mazishi unaotolewa kwa familia ya mfanyakazi
endapo mfanyakazi atafariki kutokana na ajali au ugonjwa uliotokana na
kazi pamoja malipo yanayotolewa kwa wategemezi wa marehemu.
Afisa Fedha Mwandamizi kutoka Mfuko
wa Fidia Kwa Wafanyakazi - WCF,Vicent Stephen akitoa elimu kwa wananchi
juu ya malipo kwa anayehudumia mfanyakazi aliyepata ajali au kuugua
kutokana na kazi na ambaye hawezi kujihudumia
Afisa Mahusiano wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi - WCF, Zaria Mmanga akielezea kauli mbiu ya CWF kuwa ni "Fidia Stahiki kwa wakati na maendeleo ya taifa letu" na mawasiliano zaidi namba za kupiga bure WCF ni 0800110028 au 0800110029
Afisa Utawala Afisa Mahusiano wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi - WCF,Ally Shekha akionesha picha za wafanyakazi walioumia kazini.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog