SERIKALI IMEITUMIA SALAMU ZA PONGEZI SERENGETI BOYS, NI BAADA YA KUTOA KIPIGO KWA GABON
Serikali imeipongeza Serengeti Boys kwa ushindi wa mabao 2-1 katika mechi ya kirafiki dhidi ya Gabon.
Serengeti
Boys wameifunga Gabon katika mechi iliyopigwa nchini Morocco ambako
timu hiyo imeweka kambi kujiandaa na michuano ya Kombe la Mataifa Afrika
litakalofanyika nchini Gabon.
Msemaji wa Serikali Dk, Hassan Abbas amesema serikali inaipongeza timu hiyo ya vijana chini ya miaka 17 kwa ushindi huo.
Serikali inawasisitiza vijana hao kuendelea kupambana wakiwa wamelenga kufanya vizuri na Watanzania na serikali iko nyuma yao.