ROONEY AMUELEZA MCHEZAJI MWENZAKE KUWA AMEAMUA KUONDOKA MAN UNITED
Nahodha wa Manchester United, Wayne Rooney ataondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.
Mmoja
wa wachezaji wa timu hiyo ndiye aliyevujisha siri, kwamba Rooney hana
raha na anaona ni wakati mwafaka kwake kuondoka Old Trafford kwa kuwa
hapati nafasi ya kucheza.
Kocha Jose Mourinho anaonyesha kutomuweka Rooney kama chaguo la kwanza lakini mara kadhaa, naye amekuwa akiumia.
Rooney
ambaye amecheza Man United kwa miaka 13 tokea alipojiunga nayo akiwa
kinda kutoka Everton, amekuwa akiandamwa na mamumivu ambayo pia
yamechangia akose mechi kadhaa.
Imeelezwa,
hana uhakika pia kucheza mechi ijayo ya Man United ambayo itakuwa ya
Europa League dhidi ya Anderlecht na itapigwa nchini Ubelgiji, Ahamisi.