Akizungumza na wanahabari jijini Dar, Kamanda wa Polisi Kamishna Simon
Sirro amesema katika mahojiano na mtuhumiwa huyo, amekiri kutenda kosa
hilo mnamo Machi 7 mwaka huku akidai kuwa alifikia uamuzi huo baada ya
kumfumania aliyekuwa mpenzi wake wakiwa chumbani na mwanaume mwingine
ambaye hata hivyo mwanaume huyo alifanikiwa kutoroka.