Mkutano na waandishi wa habari
Picha na Daudi Manongi
Greyson Mwase na Husna Saidi
Waziri
wa Nishati na Madini,Profesa Sospeter Muhongo amesema nishati ya uhakika ya umeme itatokomeza umasikini
nchini Tanzania ifikapo mwaka 2030.
Profesa
Muhongo aliyasema hayo alipokuwa akizindua Jukwaa la Nishati Tanzania (TEP) pamoja na mkutano wa siku mbili kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu mapema leo jijini Dar es Salaam.
Mkutano
huo unaolenga kujadili upatikanaji wa nishati endelevu ya kutosha kwa bei nafuu
kwa ajili ya uchumi wa viwanda Tanzania, unakutanisha wadau mbalimbali zikiwemo
kampuni za utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi nchini kama vile Statoil, BG na Shirika la Maendeleo ya Petroli
Tanzania (TPDC).
Wadau
wengine ni pamoja na kampuni za
kuzalisha umeme kama vile Shirika la
Umeme Tanzania (TANESCO) Songas pamoja na
mabalozi wa nchi mbalimbali,
taasisi za kifedha na viongozi wa kiserikali.
Profesa
Muhongo alisema kuwa Serikali imeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha
nishati ya uhakika inapatikana itakayopelekea Tanzania kuwa nchi ya kipato cha
kati ifikapo mwaka 2025 kama Dira ya Maendeleo ya Taifa inavyofafanua.
Profesa
Muhongo alisema kuwa nishati ya kutosha itapelekea uanzishwaji wa viwanda
vidogo hususan katika maeneo ya vijijini na kuzalisha ajira hivyo kupunguza
wimbi la vijana kuhamia mijini kutafuta maisha.
Akielezea
mikakati ya upatikanaji wa nishati ya uhakika nchini, Profesa Muhongo alisema kuwa
serikali imeandaa mpango wa matumizi ya vyanzo vya nishati ya umeme ambapo gesi
ni asilimia 40, maji asilimia 25, makaa ya mawe asilimia 30 na nishati mbadala
asilimia 5
Aliongeza
kuwa serikali inakaribisha wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi katika sekta
za nishati ili kuongeza uzalishaji wa umeme nchini.
Akielezea maendeleo ya mipango ya Serikali, Profesa
Muhongo alisema hadi sasa Serikali imeshakamilisha ujenzi wa bomba la
gesi kutoka Mtwara hadi jijini Dar es
Salaam na kuongeza kuwa ugunduzi wa gesi
ya kutosha katika mikoa ya Mtwara na Lindi umepelekea uanzishwaji wa viwanda
vya saruji na mbolea katika mikoa hiyo.
Alisema
pia serikali ipo katika hatua ya mwisho
ya majadiliano kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka
Hoima nchini Uganda hadi Tanga,
Tanzania na kusisitiza kuwa Serikali imeanza majadiliano kwa ajili ya mradi wa
bomba la kusafirisha mafuta kutoka
jijini Dar es Salaam hadi Ndola, Zambia.
Aliendelea
kusema kuwa Serikali imekuwa ikikutana na wawekezaji kutoka kampuni za utafiti na uchimbaji wa mafuta na
gesi nchini kila baada ya miezi mitatu
ili kufahamu maendeleo na changamoto ya shughuli zake.
Aliendelea
kutaja mipango mingine kuwa, ni pamoja na uanzishwaji wa kozi mbalimbali katika
masuala ya gesi na mafuta katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo
Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Waziri
Muhongo alisema kuwa Serikali imekuwa ikitoa ufadhili kwa wataalam wake kwa
ajili ya kusomea masuala ya gesi na mafuta
katika ngazi ya shahada za uzamili na uzamivu katika vyuo vikuu mbalimbali nje
ya nchi.
Aidha,
aliongeza kuwa serikali kupitia balozi
mbalimbali imekuwa ikitoa ufadhili kwa wanafunzi wanaofanya vizuri katika
masomo ya sayansi kusomea masuala ya gesi katika vyuo vya ndani na nje ya nchi.
“Lengo
letu kama Serikali, ni kuhakikisha kuwa tunazalisha wataalam wa kutosha
watakaofanya kazi katika kampuni za mafuta na gesi na hivyo kuinua uchumi wa
nchi,” alisisitiza Profesa Muhongo.
Naye
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam (UDSM), Florens Luoga alisema kupitia Jukwaa la Nishati Tanzania linaloundwa na wataalam kutoka Tanzania na Uholanzi wanaangalia namna ya
kushirikiana kupitia kubadilishana uzoefu kupitia program mbalimbali.
Mkutano
huo unaoambatana na maonesho ya kampuni
mbalimbali za utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi pamoja na kampuni za
uzalishaji wa umeme umeandaliwa na Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa
kushirikiana na Taasisi ya Teknolojia na
Sayansi ya Kar
|