MKENYA WANJIRU AONYESHA SI MCHEZO KWA KUSHINDA LONDON MARATHON MBELE YA BEKELE WA ETHIOPIA
Mkenya Daniel Wanjiru ameshinda mbio za
London Marathon na kumuacha mkali wa mbio hizo, Kenenisa Bekele
akichukua nafasi ya pili.
Wanjiru raia wa Kenya ameshinda kwa muda wa saa 2, dakika 5 na sekunde 48 na kuonyesha alikuwa vizuri mbele ya Bekele.
Bekele ndiye anayeshikilia rekodi ya dunia ya mbio za Mita 5000 na 10000 lakini hakuweza mkufua dafu dhidi ya Mkenya huyo.
Kikubwa alichokuwa amelenga Wanjiru ni
kuimaliza rekodi ya Mkenya mwenzake, Dennis Kimetto ya 2:02:57 lakini
hats hivyo imeshindikana ingawa ameingia kwenye kitabu cha mmoja wa
wanariadha bora kabisa kukimbia kwenye London Marathon.
Yeye na Bekele, mwishoni ilikuwa ni
ushindani mkali huku Bekele akionyesha kupunguza pengo dhidi yao lakini
Mkenya huyo, mwisho alicharuka na kushinda.