MECHI TANO, MBEYA CITY WAENDELEA KUPAMBANA NA JINAMIZI LA SARE
KIKOSI
cha Mbeya City, kimeshindwa kupata ushindi kwenye michezo mitano
mfululizo ambayo ni sawa na dakika 450 hali ambayo inaiweka njia panda
timu hiyo kwenye harakati zao za kumaliza nafasi za juu kwenye msimamo
wa Ligi Kuu Bara.
Timu
hiyo ambayo juzi Jumamosi ilifungwa mabao 2-1 na Ndanda wakiwa kwenye
uwanja wao wa nyumbani wa Sokoine jijini Mbeya, mwanzoni mwa msimu huu
iliweka mikakati ya kumaliza ligi ndani ya timu tano bora za juu.
Mbeya
City kwa sasa inashika nafasi ya sita ikiwa na pointi 32, mara ya
mwisho kupata ushindi kwenye michezo yake ya Ligi Kuu Bara ilikuwa ni
Februari 5, mwaka huu walipoifunga JKT Ruvu bao 1-0, lakini baada ya
hapo wamecheza mechi tano na kushindwa kupata ushindi.
Matokeo
ya mechi hizo yalikuwa hivi; Mwadui 3-2 Mbeya City, Stand United 0-0
Mbeya City, Simba 2-2 Mbeya City, Mbeya City 1-1 Ruvu Shooting na Mbeya
City 1-2 Ndanda ambapo wamekusanya pointi tatu kati ya pointi 15.
Kutokana
na hali hiyo, kocha wa kikosi hicho, Kinnah Phiri, raia wa Malawi,
amesema: “Matokeo si mazuri sana, lakini tunaendelea kupambana
kuhakikisha tunafikia malengo tuliyojiwekea, hali hii inaweza kuitokea
timu yoyote ile na hiyo ndiyo maana halisi ya mchezo wa soka, matokeo ya
kushangaza ni sehemu mojawapo ya changamoto.”