MASHABIKI DORTMUND WAONYESHA UUNGWANA KWA WENZAO WA MONACO, WAWAPA "UTELEZI"
Mashabiki wa Borussia Dortmund ya Ujerumani, wameonyesha ni waungwana baada ya kuwapa “utelezi” wenzao wa Monaco kutokana na kuvurugika kwa ratiba.
Watoto
wa mjini, neno utelezi linatumika kama msaada. Mashabiki wa Dortmund
wameamua kuwasaidia wa Monaco wakati timu hizo zinakutana leo mjini
Dortmund, Ujerumani.
Mechi
ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baina ya timu hizo ilipangwa kufanyika jana,
lakini basi la Dortmund likashambuliwa na watu wasiojulikana kupitia
milipuko mitatu.
Hali
hiyo imefanya Uefa, kusogeza mchezo huo mbele kwa kuwa mchezaji mmoja
wa Dortmund, Marc Bartra aliumia na kupelekwa hospitali.
Mashabiki wa Monaco wanatokea nchi jirani ya Ufaransa na Ujerumani ni jirani zao wazuri ambao wameamua kuwaonyesha uungwana huo kwa kuwachukua na kulala nao makwao na kula na kunywa nao pamoja.
Kuvurugika
kwa ratiba, kumefanya mashabiki wa Monaco waanze kuhangaika malazi na
wale wa Dortmund wameamua kuonyesha mpira ni furaha na wala si uadui,
wakawapa utelezi huo safiii.