Kumekuwa Na Mkanganyiko Wa Habari Na Upotoshwaji Wa Taarifa, Ambazo Si Sahihi Kuhusiana Na Yanga Kuchezesha
Kikosi Cha Pili Hapo Jana Dhidi Ya Kombaini Ya Majeshi Katika Uwanja Wa Jamhuri Mjini Dodoma.
Naomba Kuliweka Jambo Hili Wazi Na Kuondoa Sintofahamu Zisizo Na Msingi Na Pengine Kufunga Mjadala Huu Rasmi.
1.Week End Ya Tarehe 22 Na 23 ,Na Ya 28 Hadi 30 Tff Walitupa Ratiba Ambayo Inaonyesha Hakuna Mchezo Wowote Local League,
Au
Fa Cup.Na Ratiba Yetu Ilionyesha Tutacheza Tarehe 22 Fa Cup Dhidi Ya
Prisons Tu Kwa Kuwa Ni Kiporo,Na Ukiangalia Ni Wiki Ya Pili Sasa Ligi
Haichezwi Kutokana Na Ratiba Ya Chan Yaani Mashindano Ya Kimataifa Ya
Caf Kwa Timu Za Taifa Kwa Wachezaji Wa Ndani.
2.Baada
Ya Kupata Ratiba Ya Mapumziko Ya Wiki Mbili Bila Michezo Ya Ushindani
,Kama Viongozi Tukaona Si Busara Wachezaji Wakae Bila Michezo Ya
Kujipima Nguvu Ili Kuendelea Kujijenga Kuwa Katika Ushindani Muda Wote.
Tukaona Wiki Mbili Ni Nyingi Mno Bora Tupate Michezo Ya Kujipima Nguvu Yaani Friends Matches Katika Majuma Haya Mawili.
Tulipokea Barua Kutoka Arusha Tucheze Mechi Mbili Tarehe 29 Na 30 Dhidi Ya Madini Na Afc,Tukakubaliana Nao Pia Tutaenda Huko.
Tukapokea Barua Ya Dodoma Tucheze Tarehe 26 Tukakubali Pia.
Sasa
Tatizo Limekuja Kwa Tff Kufanya Droo Tarehe 23 ,Na Kututaka Tucheze
Tarehe 30 Nusu Fainali Ya Fa Cup Ratiba Ambayo Haikuwepo Kabla Ya Hapo
,Sisi Tulikubali Kucheza Michezo Hiyo Tukijua Hakuna Mashindano Yoyote
Ndani Ya Tarehe Hizo.
3.Nakiri Kabisa Kuwa Tatizo Limesababishwa Na Ratiba Zisizoeleweka Za Tff Tusingefika Hapo,
Kama Ratiba Ya Tff Ingekuwa Si Kukurupuka Tusingefika Hapo Leo.
Tumecheza Mechi Ya Kiporo Na Prisons Tukashinda Huku Tukiwa Na Majeruhi Wanane Key Players.
Vicent Bossou
Donald Ngoma
Haruna Niyonzima
Juma Abdul
Malimi Busungu
Ally Mustapha
Anthony Mateo
Deus Kaseke
Siku Ya Pili Ratiba Inatoka Tucheze Nusu Fainali,Narudia Tena Nusu Fainali Tucheze Ndani Ya Siku Saba.
Kwa
Vyovyote Vile Hata Ingekuwa Vipi ,Kwa Kikosi Tegemezi Cha Wachezaji 18
Tu,Kukichu Kua Na Kwenda Kukipiganisha Katika Michezo Miwili Mfululizo
Ambao Mmoja Hauna Tija Kabisa Tena Michezo Hiyo Ipishane Kwa Siku Tatu
Tu, Hii Haijawahi Fanywa Na Timu Yoyote Duniani.
4.Kwa
Kuliona Hilo Na Kwa Mapenzi Ya Dhati Kabisa Kutoka Mioyoni Mwetu
Viongozi Dhidi Ya Wapenda Mpira Wote Wa Mkoa Wa Dodoma Na Maeneo Ya
Jirani,Viongozi Kwa Pamoja Sote Tulitafakari Tukasema Kheri Ya Nusu
Shari Kuliko Shari Yenyewe.
Kwa
Pamoja Tukahamua Kupeleka Timu Ya Kikosi Cha Pili Wakichanganyika Na
Wale Wa Kikosi Cha Kwanza Ambao Hawajatumika Muda Mrefu Waungane Na
Vijana Hao Kwenda Kuwapa Burudani Wananchi Wa Kanda Ya Kati Dodoma.
5.
Nashukuru Timu Ikiongozwa Na Mimi Mjumbe Mkemi,Mjumbe Hashimu Na
Mjumbe Siza Imefika Salama Na Bado Ipo Salama Salmin Na Jana Imeonyesha
Kiwango Cha Juu Kabisa Na Wale Waliokuwa Hawaamini Waliacha Viti Vyao Na
Kushangilia Soka Safi Na Maridadi La Vijana Wa Yanga.
Mpaka Nikawatania Vijana Ni Hali Hii Wangekuja Baba Zao Ndiyo Msingekaa Vitini Muda Wote.
Kwa
Machache Ni Hayo Ila Na Peleka Pongezi Kwa Benchi La Ufundi La Yanga B
Chini Ya Kocha Shadrack Msajigwa Kwa Kiwango Bora Kabisa Cha Timu Yake
Amewapika Vizuri Hakika Hiki Ni Kikosi Hadhina Maridhawa Ya Yanga Hapo
Baadae.
Nitakuwa Mchoyo Wa Fadhila Kwa Pato Ngonyani Alikuwa Captain Jana Kiwango Kizuri Hakika Anarudi Sasa.
Yote
Katika Mwisho Pongezi Kubwa, Nzuri Sifa Kedekedee Kwa Yusuf Mhilu
Mfungaji Bao La Kusawazisha Dhidi Ya Majeshi,Siyo Sifa Hizi Kwa Ajili Ya
Goli Tu La Hasha Hakuna Aliyekaa Bila Kutoa Yowe La Furaha Kila
Aliposhika Mpira, Huyu Ni Messi Wa Tanzania Kwa Vizazi Vipya Vya Mpira
Tanzania.
Mwisho
Kabisa Naliomba Shirikisho La Mpira Tanzania (TFF), liwe Linatoa
Kalenda Au Ratiba Ambazo Baadae Hazitaleta Mitafaruku Kama Hii Hapo
Baadae .
Yanga Oyeee
Daima Mbele
Nyuma Mwiko
Salum Mkemi
Mjumbe Kamati Ya Utendaji Yanga.
Msimamizi Mkuu Wa Idara Ya Habari Na Mawasiliano Yanga.