KUTANA NA ROBOTI YENYE UWEZO WA KUPAMBANA NA WAHALIFU KWENYE MADUKA MAKUBWA
Ubunifu ndio unaiendesha dunia lakini sio kila mtu amepewa uwezo wa
kubuni bali wapo wachache kwenye kundi la wengi ambao wana uwezo wa
kubuni mambo mbalimbali ndiyo maana nimekuletea stori hii ya ubunifu wa
hali ya juu.
Kampuni ya Silicon Valley imebuni mbinu mpya ya kupambana na uhalifu
katika maduka makubwa baada ya kutengeneza robot ambayo kazi yake ni
kupambana na uhalifu katika maduka makubwa zikitengenezwa kwa teknolojia
ya hali ya juu ambapo zitafanya kazi bila usimamizi wa binadam na
kukodishwa kwa Dollar 7 (£5) ambazo ni sawa Tsh. 15,400 kwa saa.
Katika stori hii iliyochapishwa na mtandao wa Daily Mail April 27, 2017
ni kwamba robot inayoitwa Knightscope K5 ina urefu wa futi 5 ni maalum
kufanya patrol katika maduka makubwa, viwanja vya michezo na kumbi za
cinema kwa lengo la kuhakikisha usalama wa maeneo hayo.
Lengo kuu la kampuni hiyo ni kuzalisha maroboti wengi zaidi ambao
watasambazwa duniani kote wakikusudia kupunguza uhalifu hadi 50% ambapo
kwa mujibu wa ripoti ni kuwa wanakusudia siku moja zitumike na Polisi
katika kusaidia kupambana na uhalifu.
Mmoja wa watengenezaji wa Knightscope Stacy Dean Stephens alisema:
“Tunaanza na maeneo ya umma, hivyo tunaziruhusu kufanya patrol kwenye
maeneo kama maduka makubwa, kampasi, viwanja vya michezo na nyumba za
cinema.”