ILE ISHU YA POINTI TATU ZA FAKHI, WAANDISHI WAAMBIWA KUONDOKA ENEO LA TUKIO
Baada
ya wanachama wa Yanga na Simba kutakiwa kuondoka sehemu kinapofanyika
kikao cha Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF), sasa waandishi nao wametakiwa kuondoka eneo
hilo.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, amemuagiza mmoja wa maofisa wa TFF, Eliud Mvela kuwaambia waandishi warejee baadaye.
"Waandishi mnatakiwa kuondoka, mwenyekiti amesema hadi saa 11, mnaweza kurejea," alisema.
Waandishi walikubaliana na hilo na wengi wameahidi kurejea katika hoteli ya Protea Oysterbay ambako kikao hicho kinafanyika.
Kikao hicho ni kusikiliza rufaa ya Kagera Sugar wanaopinga Simba kupewa pointi tatu na kamati ya Saa 72.
Kamati
ya Saa 72 iliipa Simba pointi tatu baada ya kubainika beki Mohamed
Fakhi alicheza mechi ambayo Kagera waliishinda Simba kwa mabao 2-1,
lakini yeye alikuwa na kadi 3 za njano.
Kagera Sugar wameendelea kusisitiza, kwamba Fakhi alikuwa na kadi mbili za njano na si tatu.