DC RORYA MADIWANI SHIRIKIANA KATIKA KUONGEZA PATO LA HALMASHAURI
Madiwani wilayani Rorya Mkoani Mara wakiwa katika kikao cha balaza la Madiwani robo ya pili ya Mwaka 2016-2017. |
Wa kwanza kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Rorya Simon Chacha wa pili ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Rorya Albert Machiwa wakiwa katika Balaza la Madiwani. |
Kikao cha baraza la Madiwani Wilayani
rorya Mkoani Mara kimekaa hii leo kwa lengo la kujadili taarifa za kata 26
zilizopo wilayani humo katika robo ya pili ya mwaka 2016-2017 Mkuu wa wilaya ya
Rorya Simon Chacha amewataka madiwani hao
kuendelea kuimiza Waanchi wao kwa lengo la kulima chakula cha Muda mfupi
ili kuondokana na upungufu wa chakula ambao unaweza kujitokeza Mbeleni.
“Waeshimiwa madiwani nadhami hali ya
hewa munaiona hebu endelea kuimiza wananchi wajikite katika kutumia hizi mvua
ambazo zinaendelea kunyesha ili kupata chakula” alisema Simon.
Mkuu wa wilaya pia ameipongeza
Halmashauri hiyo katika suala zima la kuendelea kufanya vyema sekta ya elimu na
kusema kuwa wilaya hiyo imetunikiwa hati ya utendaji bora na waziri wa Elimu,Sayansi,
Teknologia na Ufundi Profesa Joyce
Ndalichako pamoja na fedha baada ya kufanya vizuri katika sekta ya Elimu.
Hivyo amewamba madiwani kuendelea kushirikiana vyema kama
walivyoshirikiana katika sekta ya elimu sasa washirikiane katika kukusanya
mapato ya ndani ili Rorya iendelee kutekeleza miradi ya wanachi ipasavyo.
Naye Mkurugenzi wa Wilaya hiyo Charles
Chacha amesema kuwa wanaendelea na mikakati ili kuendelea kubuni vyanzo vya
mapato kwa lengo la kuongeza kipato na kutekeleza miradi ya Wanchi katika Sekta
zote ikiwemo Afya, Maji Elimu na Barabara.
Edward Ndege ni diwani wa kata ya
Nyahongo amedai kuwa kwa sasa wilaya hiyo inakumbwa na upungufu wa chakula
hivyo wameiomba Serikali kuona haja ya kuleta chakula cha bei nafuu ili wanachi
waweze kununua huku akisema kuwa kwa sasa kuna wadudu hatari ambao
wanashambulia mahindi jambo ambalo linazidi kuwakatisha tama wanachi wao.
Hata hivyo Madiwani hao kwa nyakati
tofauti wamedai kuwa kuna wadudu ambao wameibuka na kuanza kushambulia zao la
mahindi kwani ni chakula ambacho wanategemea hivyo wameimba idara ya kilimo kuendeleza
tafiti ili kubaini wadudua hao kwa lengo la kuwatokomeza.