DC KASESELA KUWACHUKULIA HATUA KALI WAHARIBIFU WOTE WA MLIMA ULIOPO MANISPAA YA IRINGA.
Na Fredy Mgunda, Iringa
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amemtaka Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa kuwachukulia hatua watu wote waliohusika na uharibifu wa mlima uliopo Kata ya kitanzini miomboni kutokana na mlima huo kuwa ni hifadhi ya taifa.
Kasesela
alisema kuwa amesikitishwa na wananchi walivamia mlima huo na kuanza
kujenga vibanda wakati kuna maeneo mengi yapo hapa Manispaa hivyo ni
lazima hatua zichukuliwe kwa sababu saizi tunahangaika kutunza uoto wa
asili halafu watu wengine wanaharibu.
"Nimefika
katika eneo lile kweli wananchi wamevamia bila hata mimi kiongozi wa
wilaya sijui nafikiri wametumia fursa ya sikukuu hii ya pasaka kufanya
uharibu huo sitakubali kuona nakiuka maagizo ya Makamu wa Rais ya
kutunza uoto wetu wa asili"alisema Kasesela
Kasesela
amemuagiza Mkurugenzi kulifiatilia swala hilo na kukikisha inapofika
kesho saa nne Vibanda vyote viwe vimevunjwa na kuanza kupanda miti
maeneo yote yaliyokatwa miti na kuhakikisha eneo liloharibiwa linarudi
kwenye ubora wake.
"Kufikia
kesho saa nne vibanda vitakuwa vimebomolewa hatuwezi kuaharibu eneo
kama lile lazima wachukuliwe hatua kuanzia wananchi hadi viongozi
waliohusika na mpango huo kwa kuwa wananchi hawawezi kuanza wenyewe bila
kupata ruhusa kutoka kwa viongozi furani" alisema Kasesela
Lakini
Kasesela alisema kuwa atakikisha anawachukulia hatua viongozi wenye
uelewa mdogo wa namna ile kwasababu kiongozi mwenye akili na uelewa
mkubwa hawezi kuruhusu kuaharibiwa eneo hilo.
Nawaomba
wananchi wa Manispaa ya Iringa na Wilaya yote ya Iringa kuwa makini
wanapoambiwa kufanya biashara katika mazingira yaliyohifadhiwa kwa kuwa
wanaharibu mazingira makusudi na pia wanapata hasara zisizo kuwa na
maana mfano walivamia huo mlima tayari wameshapata hasara lakini wameipa
hasara kubwa serikali na jamii yote.
Uharibifu mkubwa unaofanywa katika mlima huo ukifumbiwa macho kama ilivyo ni wazi uongozi wa Manispaa ya Iringa umepuuza agizo hilo la makamu wa Rais na uwezekano wa uhifadhi wa ikolojia ya mto Ruaha kwa mwendo huo itakuwa ni ndoto ya alinacha
Uharibifu mkubwa unaofanywa katika mlima huo ukifumbiwa macho kama ilivyo ni wazi uongozi wa Manispaa ya Iringa umepuuza agizo hilo la makamu wa Rais na uwezekano wa uhifadhi wa ikolojia ya mto Ruaha kwa mwendo huo itakuwa ni ndoto ya alinacha