BENITEZ SI MCHEZO, AIREJESHA NEWCASTLE LIGI KUU ENGLAND
Kocha Rafa Benitez, amefanikiwa kuirejesha tena Newcastle katika Premier League.
Newcastle imeitwnaga Preston kwa mabao 4-1 na kufanikiwa kurejea Ligi Kuu England.
Mabao ya Christian Atsu, Matt Ritchie na Ayoze Perez yameisukuma Newcastle kwenye ligi hiyo maarufu zaidi.
Licha ya kuwa kocha mkubwa lakini
Benitez alikubali kuteremka na kurejea na timu hiyo hadi daraja la
kwanza akiwa na matumaini ya kuipandisha.