MIKAKATI YA KAMPUNI YA ACACIA KATIKA KUINUA ELIMU MKOANI SHINYANGA.

Shaban Njia
Katika kuhakikisha mkoa wa Shinyanga unaweza kufanya vema katika matokeo ya mitihani ya kumaliza kidato cha nne kwa wananfunzi wa kike, kampuni ya Acacia kupitia mgodi wake wa dhahabu wa Bulyanhulu umeanza kuwazadia wanafunzi hao pindi wanapofanya vizuri katika masomo yao.

Zawadi zitakuwa zikitolewa kila mwaka katika Maazimisho ya siku ya Wanawake Duniani na tayari kwa mwaka huu Acacia imewapatia Baskeli jumla ya  wanafunzi wa kike nane na walimu walezi wawili katika shule za sekondari za Bugarama na Bulyanhulu waliofanya vizuri katika masomo yao.

Akikabidhi Baskeli hizo juzi Afisa Mahusiano wa mgodi huo Zuwena Sekondo, alisema kuwa baskeli hizo zitasaidia kuwatia hamasa wananfunzi wa kike hasa wale wanatumia umbali mrefu kutoka majumbani kwao kwenda shule kuendelea kufanya vema katika mitihani ya shule pamoja na ile ya kitaifa.

Sekondo aliwataja waliozawadiwa Baskeli hizo katika Sekondari Bulyanhulu ni Irene Jimmy wa kidato cha tatu aliyeshika  nafasi ya kwanza katika mitihani wa kidato cha pili mwaka jana,huku Zainabu Kisambale wa kidato cha tatu akifanya vizuri  katika mihati yake ya kidato cha pili kwa kupata daraja la pili.
Wengine ni Maombi Silvester aliyeshika  nafasi ya kumi katika mitihani yake na kuendelea kuonesha nidhamu huku Rehema Abdallah  wa kidato cha nne akishika nafasi ya kumi katika mitihani ya shule na pia  mwaka jana akiwa kidato cha tatu alishika nafasi ya tatu.

Aidha Sekondo aliendelea kuwataja wanafunzi wa kike walipata baskeli katika sekondari ya Bugarama kuwa ni Jeschal Peter kidato cha kwanza anaefanya vizuri katika somo la kingereza ,Rozi Juma Omary kidato cha pili aliyeshika ya kumi katika mitini wa kitaifa mwaka jana.

Pia aliwataja pia  Philomena Achoro kidato cha pili aliwahi kushika nafasi ya kwanza akiwa kidato cha kwanza mwaka jana,Evelini Silasi kidato cha nne aliwahi kushika nafasi ya sita akiwa kidato cha tatu mwaka jana pamoja na mwalimu wao mlezi Priscal Mwanantemi.

Hata hivyo aliyataka mashirika ya kiserikali na yale yasiyo ya kiserikali kujitoa katika kumpigania mtoto wa kike katika kupata elimu hali ambayo isaidia mtoto wa kike kujiongoza katika maisha yake ya baadae nakuongeza kuwa kutasaidia kupunguza wimbi la wanawake wasio na elimu.
Katika hatua nyingine kampuni ya Acacia imetoa mashuka, sabuni, dawa ya meno pamoja na Mafuta kwa wagonjwa wa  Wanawake na Wanaume  katika kituo cha Afya cha Bugarama na Lunguya lengo likiwa ni kupambana na wimbi la uchafu katika vituo vya afya katika Halmashauri ya Msalala.

Sekondo alisema kuwa suala la kutoa sabuni,mafuta pamoja na mashuka sio la mgodi pekee ni jukumu la kila mtanzania kujitoa kuwasaidia wagonjwa wasio jiweza waliko katika Hospitali na Vituo vya afya vilivyopo karibu yao.

Afisa tabibu kutoka katika kituo cha afya cha Lunguya, John Malango, alisema kuwa kutokana na msaada uliotloewa na mgodi wa Bulyanhulu utasaidia kuboresha huduma ya usafi wa mazingira ya kituo hicho na kuwataka watu wengine kujitokeza katika kuboresha huduma za kiafya.
Powered by Blogger.