ASKOFU GWAJIMA APEKULIWA NA POLISI TENA
Kibatala
ambaye ni wakili wa Askofu Gwajima amesema kuwa mbali na kupekuwa
nakupiga picha kila kona ya nyumba pia walikwenda katika kanisa lake
lililopo Ubungo kwa ajili ya upekuzi.
“Waache
wafanye yao na sisi tutafanya yetu kisheria, Kwani hatuwezi kuwazuia
Polisi kufanya shughuli yao na baada ya kumaliza na sisi tutajua nini
cha kufanya,” amesema Kibatala.
Msemaji
wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, David Mngongolwa amesema Gwajima
alikwenda polisi kuripoti kama alivyoamriwa kufanya hivyo.
Aidha,
Mngongolwa ameongeza kuwa baada ya kuripoti askari walimchukua na
kwenda naye nyumbani kwake kwa ajili ya upekuzi na baada ya hapo
waliondoka naye.
Hata
hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Suzan Kaganda
amesema hana taarifa za kukamatwa kwa Gwajima kwa maelezo kuwa alikuwa
katika kikao.