Waziri Mkuu, Mawaziri Kuongoza Mapambano Dawa Za Kulevya

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimvalisha cheo kipya aliyekuwa Mkuu wa Chuo cha Uhamiaji Mkoani Kilimanjaro Dkt. Anna Peter Makakala kabla ya kumuapisha kuwa Kamishna Mkuu wa Uhamiaji Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha aliyekuwa Mkuu wa Chuo cha Uhamiaji Mkoani Kilimanjaro Dkt. Anna Peter Makakala kuwa Kamishna Mkuu wa Uhamiaji Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini hati ya kiapo baada ya kumuapisha Dkt. Anna Peter Makakala kuwa Kamishna Mkuu wa Uhamiaji Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi vitendea kazi Dkt. Anna Peter Makakala baada ya kumuapisha kuwa Kamishna Mkuu wa Uhamiaji Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bw.Rogers William Sianga kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya Bw.Rogers William Sianga akisaini hati ya kiapo baada ya kuapishwa Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini hati ya kiapo baada ya kumuapisha Bw.Rogers William Sianga kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi vitendea kazi Bw.Rogers William Sianga baada ya kumuapisha kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Omar Yusuf Mzee baada ya kumteua kuwa balozi Leo Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Joseph Sokoine baada ya kumteua kuwa balozi Leo Jijini Dar es Salaam.

Viongozi walioapishwa leo Ikulu Jijini Dar es Salaam wakila kiapo cha Maadili katika utumishu wa umma kilichoongozwa na Kamishna wa Maadili katika Sekretariat ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Mhe. Jaji Harold Nsekela
Kamishna wa Maadili katika Sekretariat ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Mhe. Jaji Harold Nsekela akiongoza kiapo kwa mabalozi na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya waliopishwa leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Mabalozi na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya waliopishwa leo Ikulu Jijini Dar es Salaam wakisaini kiapo cha Maadili katika utumishu wa umma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa Hafla ya kuwaapisha Mabalozi na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya waliopishwa leo Ikulu Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa Hafla ya kuwaapisha Mabalozi na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya waliopishwa leo Ikulu Jijini Dar es Salaam
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akiongea na viongozi mbalimbali wa serikali waliohudhuria halfa ya uapishwaji wa Mabalozi na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya ambapo alisisitiza umuhimu wa viongozi wa serikali pamoja na wananchi kuungana kwa pamoja katika mapambano dhidi ya biashara haramu ya Dawa za kulevya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na viongozi mbalimbali wa serikali waliohudhuria halfa ya uapishwaji wa Mabalozi na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya ambapo aliwataka watanzania na viongozi wenye mamlaka ya kupambana na dawa za kulevya kufanya hivyo ili kuweza kuinusuru Tanzania dhidi ya uingizwaji na uendeleaji wa biashara haramu ya dawa za kulevya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mawaziri waliohudhuria hafla ya uapishaji wa Mabalozi na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha pa pamoja na Mabalozi na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya walioapishwa leo Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri na Makatibu Wakuu baada ya kuwaapisha Mabalozi na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya Ikulu Jijini Dar es Salaam.
PICHA NA HASSAN SILAYO





Jacquiline Mrisho na Eliphace Marwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemkabidhi Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa kazi ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya akiwa kama Mwenyekiti wa Tume ya Kudhibiti Dawa hizo nchini.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam wakati akiwaapisha Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji, Anna Peter Makakala, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers William Sianga pamoja na mabalozi watatu Mhe. Omary Yusuph Mzee, Mhe.Joseph Edward Sokoine pamoja na Mhe. Grace Aron Mgovano aliowateua hivi karibuni.
Dkt. Magufuli amesema kuwa Waziri Mkuu anatajwa kwenye Sheria Na.5 ya mwaka 2015 kuwa ni Mwenyekiti wa Tume hiyo ambapo Wajumbe wake ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Waziri wa Mambo ya Ndani, Waziri wa Elimu ana Mafunzo ya Ufundi, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Waziri wa Fedha na Mipango, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
“Nalipongeza sana Bunge la kipindi cha mwaka 2010 – 2015 chini ya Spika mstaafu, Mhe. Anne Makinda lililopitisha Sheria hii baada ya kuona sheria za mwanzo za kupambana na dawa za kulevya hazina nguvu hivyo Wabunge wa wakati ule walisimama kwa pamoja bila kujali itikadi za vyama vyao wakapitisha sheria hii,” alisema Dkt. Magufuli.
Aidha, Dkt. Magufuli amempongeza Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete kwa kusaini sheria hiyo haraka mara baada ya Bunge hilo kuipitisha kwa sababu alijua madhara ya dawa za kulevya katika nchi yetu.
Amefafanua kuwa sheria imeeleza wazi katika kifungu cha 10 cha Sheria Na.5 ya mwaka 2015 kuwa jukumu la kupambana na dawa za kulevya linasimamiwa na Serikali pekee yaani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Makamo wa Rais, Waziri Mkuu, Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Wilaya pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya au mtu yoyote atakayekuwa amepewa mamlaka ya kusimamia Serikali.
Kwa upande wake Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa amesema kuwa Taifa limeendelea kushuhudia kizazi chetu kikiendelea kudidimia kwa sababu ya matumizi ya dawa za kulevya na Serikali kwa mipango yake imeendelea kukemea, kudhibiti na kuchukua hatua mbalimbali dhidi ya wazalishaji, wasambazaji, wauzaji na watumiaji wa dawa hizo.
“Jambo hili limeleta athari kubwa sana kwani vijana wetu wengi wamepoteza uwezo wa kujisimamia katika shughuli zao za maendeleo kwa sababu baada ya matumizi tumeona athari kadhaa zikiwezo za kudhoofishwa kwa mwili, uwezo wa kutafakari pamoja na kutoweka kwa uwezo wa kufanya kazi,”alisema Waziri Mkuu Majaliwa.
Waziri Mkuu Majaliwa ameongeza kuwa Taifa hili la Watanzania kwa kiasi kikubwa linawategemea vijana waweze kuleta msukumo wa maendeleo ndani ya nchi hivyo jambo hili likiachiwa linaweza kuleta athari kubwa katika ukuaji wa uchumi na maendeleo yetu kwa ujumla wake.
Alisisitiza kuwa vita hii ilianza, inaendelea na itaendelea kupiganwa hadi imalizike hivyo Watanzania hawana budi kuunga mkono jitihada zozote zinazofanywa na Serikali kuhakikisha wanatokomeza uzalishaji, usambazaji, uuzaji na matumizi yake kwa namna yoyote ile, kila mmoja anatakiwa kushiriki kikamilifu ili kubaini matumizi ya dawa za kulevya ndani ya nchi hii.
Powered by Blogger.