WATUHUMIWA 17 WA DAWA ZA KULEVYA WAKAMATWA SHINYANGA...MAJINA MENGINE ZAIDI YA 20 YAPO KWA DC SHINYANGA
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine
Matiro akitoa taarifa kwa waandishi wa habari leo (hawapo pichani)
Alhamis Februari 9,2017 kuhusu kukamatwa kwa watuhumiwa wa dawa za
kulevya katika wilaya ya Shinyanga-Picha na Kadama Malunde-Malunde1
blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine
Matiro akielezea jinsi wananchi wa wilaya hiyo waliamua kuchukua hatua
ya kupeleka majina ya watumiaji na wauzaji wa dawa za kulevya wilayani
humo
Mkuu wa polisi wilaya ya Shinyanga Dotto
Mdoe akielezea kuhusu kikosi kasi walichounda kufuatilia majina ya watu
wanaotajwa kuhusika na dawa za kulevya wilayani humo
******
Vita dhidi ya dawa za kulevya imetua
mkoani Shinyanga ambapo jumla ya watu 17 wanaotuhumiwa kuwa ni
watumiaji wa dawa hizo ikiwemo unga na mirungi wanashikiliwa na jeshi la
polisi wilaya ya Shinyanga.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro,ambaye pia ni mwenyekiti
wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya hiyo amesema mbali na watu 17
kushikiliwa na polisi pia ofisi yake imepokea majina zaidi ya 20 ya watu
wanaodaiwa kujihusisha na dawa za kulevya.
“Mheshimiwa rais ametangaza kuwa hii ni
vita ya nchi nzima,baada ya wananchi kusikia vita ya dawa za kulevya
ikiendelea mkoani Dar es salaam,wametuletea majina zaidi ya 20 ya watu
wanaojihusisha na dawa za kulevya,wanasema wanaunga mkono jitihada
zinazofanywa na serikali kupiga vita dawa hizi”,amesema Matiro.
“Wananchi wenyewe kwa moyo mweupe kabisa
ndiyo wametuletea majina ya watu wanaotumia na kuuza dawa za kulevya
ikiwemo unga na mirungi,kamati ya ulinzi na usalama tumeunda kikosi kazi
cha kushughulikia majina yanayoletwa ili kubaini kama ni kweli
wanajihusisha na dawa za kulevya”,alisema Matiro.
Ametumia fursa hiyo kulipongeza jeshi la
polisi kwa jitihada zake dhidi ya dawa za kulevya na kufanikisha
kukamata watuhumiwa 17 huku akikisisitiza kuwa vita hiyo siyo ya Dar es
salaam pekee bali inatakiwa kufanyika nchi nzima kwani watumiaji na
wauzaji wa dawa hizo wapo kila mahali nchini.