NAPE: REDIO ZIENDANE NA UKUAJI WA TEKNOLOJIA YA HABARI
Picha na Habari na Raymond Mushumbusi
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amevishauri vyombo
vya habari nchini hususani Redio kuendana na mabadiliko ya Teknolojia ya Habari
na Mawasiliano inayokuwa kwa kasi.
Ameyasema
hayo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yaliofanyika katika Chuo
Kikuu huria cha Tanzania na kusisitiza vyombo vya habari nchini hasa Redio
kuendana na mabadiliko ya ukuaji wa Teknolojia ili kuenda sambamba na
mabadiliko hayo.
Ameongeza
kuwa Redio nchini zinatakiwa ziandae mikakati zaidi ya kuendana na mabadiliko
hayo kwani ndio sasa dunia inapoelekea.
“Kutokana
na mabadiliko ya Teknolojia mtu anaweza kurekodi tukio na kuliweka mtandaoni
muda huo huku redio ikisubiri kuandika na kuhariri tukio hilo na kulirusha
hewani tuliangalie hili kwa kina” Alisisitiza Mhe. Nnauye.
Amewasahuri
waandishi wa habari nchini kuwa natabia za kusoma na kujua Taratibu na Sheria
mbalimbali zinaendesha tasnia yao ili kuifanya tasnia kukua na kujengeka.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayub Riyoba
amesema kuwa vyombo vya habari nchini hususani Redio vinatakiwa kuendana na mabadiliko
ya teknolojia inayokua siku hadi siku ili kuleta tija katika utoaji habari
kupitia Redio.
“Ndugu
zangu wanahabari hasa wale kwenye Redio tuendane na mabadiliko ya teknolojia
kwani Redio ni moja ya chombo cha mawasiliano kinachowafikia watu wengi kwa urahisi”
Alisistiza Dkt Riyoba.