|
Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniphace
Simbachawene akizungumza wakati wa mkutano baina yake na wajumbe wa Kamati ya
Uongozi wa MKURABITA Ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam kwa lengo la
kuwasilisha taarifa ya tathimini ya utekelezaji wa Mpango wa Urasimishaji wa
Rasilimali na Biashara katika Halmashauri nchini.Kushoto ni Mwenyekiti wa
Kamati ya Uongozi wa Mkurabita Kapteni Mstaafu John Chiligati.
|
|
Mwenyekiti wa Kamati
ya Uongozi wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara Tanzania (MKURABITA)
Mhe. Kapteni Mstaafu John Chiligati akielezea jambo wakati wa kikao baina ya
kamati hiyo na TAMISEMI kuhusu tathmini ya utekelezaji wa mpango huo katika
Halmashauri mbalimbali nchini leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka Kulia ni Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.
George Boniphace Simbachawene, Mratibu wa MKURABITA Bibi. Seraphia Mgembe na
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa MKURABITA Profesa. Aldo Lupala.
|
|
Mratibu wa MKURABITA Bibi.
Seraphia Mgembe akifafanua jambo wakati wa kikao baina ya Kamati ya Uongozi ya
MKURABITA na TAMISEMI kuhusu tathmini ya utekelezaji wa mpango huo katika
Halmashauri mbalimbali nchini leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka Kulia ni Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.
George Boniphace Simbachawene, Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mpango wa
Kurasimisha Rasilimali na Biashara Tanzania (MKURABITA) Mhe. Kapteni Mstaafu
John Chiligati na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa MKURABITA Profesa.
Aldo Lupala.
|
|
Watendaji kutoka
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambao ni
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Miji Dkt. Mkuki Hante pamoja na Mkurugenzi wa
Utawala kwa Serikali za Mitaa Bibi. Miriam Mmbaga wakifuatilia mjadala wakati
wa kikao baina ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI na MKURABITA kuhusu
tathmini ya utekelezaji wa mpango huo leo Jijini Dar es Salaam.
|
|
Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniphace
Simbachawene akipokea taarifa ya tathmini kuhusu utekelezaji wa Mpango wa
Kurasimisha Rasilimali na Biashara uliofanyika katika Halmashauri 52 na Miji 9
nchini kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mkurabita Kapteni Mstaafu
John Chiligati leo Jijini Dar es Salaam.
|
|
Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniphace
Simbachawene akipokea taarifa ya tathmini kuhusu utekelezaji wa Mpango wa
Kurasimisha Rasilimali na Biashara uliofanyika katika Halmashauri 52 na Miji 9
nchini kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mkurabita Kapteni Mstaafu
John Chiligati leo Jijini Dar es Salaam.
|
|
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniphace Simbachawene akisoma taarifa
ya tathmini kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Kurasimisha rasilimali na biashara
uliofanyika katika Halmashauri 52 na Miji 9 nchini mara baada ya kuipokea kutoka
kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mkurabita Kapteni Mstaafu John Chiligati(hayupo
pichani) leo Jijini Dar es Salaam |
|
Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniphace
Simbachawene akiteta jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mkurabita
Kapteni Mstaafu John Chiligati (katikati) Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya
Uongozi wa MKURABITA Profesa. Aldo Lupala mara baada ya mkutano baina yake na wajumbe wa Kamati ya hiyo
Ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam.
Na: Mpiga Picha Wetu.
|
Na:
Frank Shija
Kufuatia
kusuasua kwa utekelezaji na maendeleo ya Mpango wa Urasimishaji wa Rasilimali
na Biashara Serikali imeziagiza Halmashauri zote nchini ambazo zimefikia na
mpango huo kuwasilisha taarifa rasmi.
Agizo
hilo limetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa Mhe. George Boniphace Simbachawene katika kikao baina yake na wajumbe
wa Kamati ya Uongozi wa MKURABITA kilichofanyika Ofisini kwake leo Jijini Dar
es Salaam.
Simbachawene
amesema kuwa TAMISEMI ni mdau muhimu katika Mpango huo wa urasimishaji wa
rasilimali hivyo ujio wa kamati hiyo kutaka kushirikiana na Tawala za Mikoa ni
jambo jema.
“Binafsi
ni muumini wa muda mrefu wa mpango huu wa urasimishaji, niseme tu mmechelewa
kuja sehemu husika kwa bila dhana ya ugatuaji wa madaraka kwa wananchi
kufanikiwa kwa mpango huu itakuwa ni adithi sasa tutaenda pamoja ili kiutimiza
azma ya mpango huu,”alisema Simbachawene.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya MKURABITA Kapteni wa Jeshi Mstaafu
John Chiligati amesema kuwa pamoja na kuwepo kwa Halmashauri zaidi ya 100
nchini mpaka sasa utekelezaji wa mpango huo umezifikia takribani Halmashauri 52
na Miji 9 tu hivyo kasi yake bado hairidhishi.
Aliongeza
kuwa changamoto wanazokumbana nazo katika utekelezaji wa mpango huo ni
Halmashauri kuuona mpango huo kama hawahusiki nao hali inayopelekea kushindwa
kuendelea pindi mwakilishi wa Mkurabita atakapo ondoka katika eneo husika.
Chiligati
amesema kuwa baada ya kubaini changamoto hiyo waliamua kuwa na makubaliano
maalum na TAMISEMI juu ya utekelezaji wa pamoja wa mpango huo jambo ambalo
wanaendelea kulifanyia kazi.
MKURABITA
ni miongoni mwa jitihada za serikali katika kuwezesha jamii kiuchumi. MKURABITA
imeanzishwa na Serikali ya Tanzania mwaka 2004 kwa lengo la kuwapa nguvu ya
kiuchumi wananchi kwa kuwaongezea uwezo wa kumiliki na kufanya biashara katika
mfumo rasmi unaozingatia utawala wa sheria. Mpango huu unasimamiwa na
kuratibiwa na Ofisi ya Rais, Ikulu.