YANGA YASULUBIWA TENA...YAGONGWA NNE TENA MAPINDUZI CUP
Yanga imeendelea kusulubiwa kwenye mashindano ya Mapinduzi Cup baada ya
kujikuta ikichezea kichapo kutoka kwa Simba kwenye mchezo wa nusu
fainali ya pili kwa mikwaju ya penati 4-2 kufuatia dakika 90 kumalizika
bila timu hizo kufungana.
Baada kichapo cha 4-0 kutoka kwa Azam FC, Yanga imeondoshwa kwenye
michuano hiyo na kuziacha Simba na Azam zikutane kwenye mchezo wa
fainali ambao utachezwa siku ya Ijumaa January 13, 2017 ikiwa ni siku
moja baada ya kilele cha Mapinduzi ya Zanzibar.
Golikipa wa Simba Daniel Agyei ndio alikuwa shujaa kwa upande wa Simba hususan kwenye changamoto ya mikwaju ya penati.
Agyei ameokoa penati mbili za Deogratius Munishi na Mwinyi Haji huku
yeye akifunga penati yake baada ya Mkude kufunga ya kwanza.
Wachezaji wa Simba waliofunga penati: Jonas Mkude, Daniel Agyei, Mzamiru Yassin na Javier Boukungu
Method Manjale ni mchezaji pekee wa Simba aliyekosa penati ambayo iliokolewa na golikipa wa Yanga Deogratius Munishi.
Simon Msuva na Thaban Kamusoko ndio wachezaji pekee wa Yanga waliofunga
penati zao huku Deogratius Minish ‘Dida’ na Mwinyi Haji penati zao
zilitua kwenye mikono ya golikipa wa Simba Daniel Agyei.